Kikao cha wawakilishi wa taasisi za Qur'ani chafanyika Madrid

Kikao cha wawakilishi wa taasisi za Qur'ani chafanyika Madrid

articoli correlati

Kikao cha wawakilishi wa taasisi za Qur'ani Tukufu kilifanyika Alkhamisi iliyopita huko Madrid mji mkuu wa Hispania.
Kwa mijibu wa tovuti ya Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu ISESCO, lengo la maudhui zilizojadiliwa katika kikao hicho, na ambazo ziliandaliwa kwa ushirikiano wa ISESCO na Jumuiya ya Kimataifa ya Hifdhi ya Qur'ani pamoja na Jumuiya ya Qur'ani ya Hispania, lilikuwa ni kuimarisha ratiba za masomo ya Qur'ani barani Ulaya.
Washiriki wa kikao hicho wamesisitiza juu ya umuhimu wa kuimarishwa mipango yamasomo ya Qur'ani barani Ulaya. Wametaka pia kuasisiwa madrasa, shule na vituo vya masomo ya Kiislamu barani humo.
Vilevile washiriki wameelezea azma yao ya kuunga mkono juhudi zinazofanyika kwa lengo la kuasisiwa taasisi muhimu ya Kiislamu pamoja na uimarishwaji wa masomo ya Qur'ani barani Ulaya.

Commenti

Lascia un tuo commento

* I campi contrassegnati con l'asterisco sono obbligatori certamente avere valore.