Harakati za Qur’ani hupunguza uhalifu wa kijamii

Harakati za Qur’ani hupunguza uhalifu wa kijamii

مقالات مرتبط

Kuzingatia masuala ya kidini, kimaadili na elimu ya jamii ya vijana pamoja na kuwekeza katika harakati za Qur’ani ni njia muafaka ya kupunguza uhalifu wa kijamii.

Ripoti ya Shirika la Habari la Ahlul Bayt(a.s)-ABNA- Kuzingatia masuala ya kidini, kimaadili na elimu ya jamii ya vijana pamoja na kuwekeza katika harakati za Qur’ani ni njia muafaka ya kupunguza uhalifu wa kijamii.

Hayo ni kwa mujibu wa Danesh Sefatzadeh mkurugenzi wa magereza katika mkoa wa Hormozgan nchini Iran. Amesema matatizo mengi ya kijamii yanatokana na kutozingatiwa mafundisho ya kidini na Qur’ani.

Amesema kuwa idadi ya wafungwa itapungua iwapo thamani za kidini zitaenezwa katika jamii.

Sefatzadeh ameashiri nafasi ya Qur’ani Tukufu na utekelezwaji mafundishi yake katika maisha ya kila siku na kusema, hiyo ndio njia bora zaidi ya kupunguza matatizo ya kijamii.

Amesema kuwa kumekuwepo na vikao 4000 vya kuhitimisha Qur’ani katika magereza ya Hormozgan mbali na kuwepo mafunzo ya tajweed, qiraa, tafsiri, sheria za Kiislamu, akhlaqi na kuhifadhi hadithi.

 


نظرات

ارسال نظر

* فیلدهای ستاره دار حتما بایستی مقدار داشته باشند.