kushinda nafasi ya kwanza ya mashindano ya Qur'ani nchini Russia

kushinda nafasi ya kwanza ya mashindano ya Qur'ani nchini Russia

مقالات مرتبط

Palestina imenyakua nafasi ya kwanza ya mashindano ya kimataifa ya kiraa na tajwidi ya Qur'ani Tukufu ambayo yalifanyika hivi karibuni mjini Moscow, Russia.

Ripoti ya Shirka la habari la Ahlul Bayt(a.s)-ABNA- Imeeleza kuwa  Kwa mujibu wa matokeo yaliyotangazwa hapo jana Jumatatu, Said Dawoud mwenye umri wa miaka 28, mwakilishi wa Palestina katika mashindano hayo alishinda nafasi ya kwanza akifuatiwa na wawakilishi wa nchi za Morocco na Saudia Arabia.

Maonyesho ya kaligrafia ya Kiislamu pia yaliandaliwa pambizoni mwa mashindano hayo. Mashindano hayo yaliyofanyika katika ukumbi wa jumba la Kosmos mjini Moscow yalidhaminiwa na kuandaliwa kwa ushirikiano wa Idara ya Masuala ya Kidini ya Waislamu ya Russia na Wizara ya Mambo ya Nje ya nchi hiyo. Nchi 35 ikiwemo Jamhuri ya Kiislamu ya Iran Italia, Russia, Uingereza, Ugiriki, Belgium Misri, Jordan, Kuwait na Afrghanistan zilizishiriki kwenye mashindano hayo yaliyoanza siku ya Jumapili.

Akizungumza baada ya kumalizika mashindano hayo, Rawa Ain Deen, Mkuu wa Baraza la Mamufti wa Russsia amesema kuwa duru ya 12 ya mashindano hayo imefanyika kwa mafanikio na kuongeza kwamba yaliwashirikisha washiriki wengi zaidi kutoka nchi mbalimbali za dunia. Ameishukuru Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwa kusaidia kufanyika kwa mafanikio mashindano hayo ya kimataifa na kuwa yamekuwa na athari kubwa kwa Waislamu wa Russia.

نظرات

ارسال نظر

* فیلدهای ستاره دار حتما بایستی مقدار داشته باشند.