Saudia arabia na washirika wake wakubali kusimamisha vita Yemen

Saudia arabia na washirika wake wakubali kusimamisha vita Yemen

Saudia arabia na washirika wake wakubaliana na wapiganaji wa Kihuthi kusimamsha vita katika mji muhimu wa bandari wa Hodeida

Shirika la habari la ABNA linaripoti kuwa: Saudia arabia na washirika wake wakubaliana na wapiganaji wa Kihuthi kusimamsha vita  katika mji muhimu wa bandari wa Hodeida. Katibu mkuu wa Umoja wa mataifa Antonio Guterres amesema makubaliano hayo yanahusiana pia na kuhamishiwa vikosi vya pande zote mbili. Mjumbe wa Umoja wa Mataifa Martin Griffiths amesema vikosi vya pande zinazohasimaiana vitaondoka Hodeida katika siku chache zijazo, na baadaye kutoka mji mkuu, ambako majeshi ya muungano wa waarabu na Marekani yamekuwa yakifanya mauaji ya kinyama. Kuondoka kwa vikosi kutaijumuisha pia bandari ya Salif inayotumiwa kwa usafirishaji wa nafaka na ile ya Ras Isa inayotumiwa kwa usafirishaji wa mafuta, ambazo zote mbili ziko chini ya udhibiti wa wapiganaji wa Houthi.

Mwisho wa habari / 291

maoni

Acha Maoni

*Mashamba alama ya asteriski ni hakika kuwa thamani.