Jordan yazuia kutoa adhana na sala ya Ijumaa kwa vipaza sauti

Jordan yazuia kutoa adhana na sala ya Ijumaa kwa vipaza sauti

Waziri wa masuala ya Waqfu na mambo ya kiimani nchini Jordan kwa mara ya kwanza katika historia ya taifa hilo ametoa amri ya kuacha kutoa Adhana na hutuba ya sala ya Ijumaa kwa vipaza sauti

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: waziri wa masuala ya Dini nchini Jordan ametoa amri ya kuzuia utoaji wa Adhana na hutuba ya sala ya Ijuma pia sala tano za kila siku katika misikiti ya nchini humo.
Hayo yamenukuliwa na tovuti ya Gazeti la Raialyoum katika ripoti zake kuwa: “Abdunnasir Abulbasal” ambaye ni waziri wa Waqfu na masuala ya Kidini nchini Jordan kwa mara ya kwanza nchini humo, amezui kutolewa kwa Adhana ya Ijumaa na hutuba yake akadhalika adhana na sala za kila siku kwa vipaza sauti za nje nchini humo.
Aidha pasina kubainisha sababu ya kutoa amri hiyo, ametoa maangizi kwa wasimamizi wote wa masuala ya Dini nchini humo kuhakikisha wanasimamia utekelezaji wa amri katika sehemu zote za ibada nchini humo.
Katika amri alioitoa imenukuliwa kama ifuatavyo: kutumia vipaza sauti vya nje ya Msikiti “kwa kutoa sauti ya hutuba ya sala ya Ijumaa” kwa kuwasikilizisha watu mwanzo wa hutuba ya Ijumaa mpaka mwisho wake alkadhalika sala za kila siku, kuanzia leo si ruhusa, hivyo watu wanapaswa kutosheka na vipaza sauti vitakavyotumiwa ndani ya Msikiti tu.

maoni

Acha Maoni

*Mashamba alama ya asteriski ni hakika kuwa thamani.