MCHANGO WA UISLAMU KATIKA MAENDELEO YA MWANADAMU SEHEMU YA KWANZA

MCHANGO WA UISLAMU KATIKA MAENDELEO YA MWANADAMU SEHEMU YA KWANZA

MCHANGO WA UISLAMU KATIKA MAENDELEO YA MWANADAMU

Katika maelezo mafupi namna hii haiwezekani kuwepo kwa suala la kutaka kuorodhesha namna ambavyo utamaduni wa Kiislamu ulivyochangia katika maendeleo ya ustaarabu wa mwanadamu

Hatuna njia ila kutaja japo kwa uchache tu wa ugunduzi muhimu uliotokana na vipaji vya watafiti wa Kiislamu na pia

kutaja wachache kati ya wasomi, wanafalsafa na waandishi wa kiislam walioongeza hamasa katika elimu ya sayansi na

fasihi, na kuzivuta fikra za watu wa Magharibi (wazungu).

Unajimu (Astronomy) Elimu ya Anga na Sayari:

Elimu na sayansi za kwanza kuvuta shauku ya wasomi wa Kiislam zilikuwa ni unajimu na Hisabati. Fikra zao zote bila

ya shaka na mweleko wao uliwafanya Waislam kuiendea sayansi ya uhakika.

Unajimu hasa sio tu uliwavutia wanasayansi, bali pia Makhalifa wa Mashariki na wa Magharibi kutoka Hispania na wa

Kirusi na Makhan wa Kihindi pia walivutiwa na taaluma hii. Vituo vyya uchunguzi wa anga vilianza kujengwa katika

kila mji maarufu katika Himaya ya Kiislam. Vile vya jiji la Baghdad, Cairo, Cordova, Toledo na Samarkand vilijipatia

umaarufu sana duniani.

Chuo cha Unajimu cha Baghdad kilijulikana tangu enzi za utawala wa AL-Mansur, Khalifa wa pili wa ukoo wa Abbassid

aliyetawala miaka ya 754 na 775, na ambaye pia alikuwa mnajimu. Hata wakati wa tawala za warithi wake, Harun al-

Rashid na AL- Mamun. Chuo hiki kiliendelea kutoa kazi nzuri.

Nadharia za zamani zilidurusiwa na makosa kusahihishwa na pia Majedwali ya Kigiriki yalisahihishwa. Chuo cha Baghdad

kinastahili sifa kwa ugunduzi wa mizunguko ya sayari na jua, tathmini ya upotofu uliokuwepo juu ya umbile lake na

utaratibu wa upunguaji wa mmuliko (ukali wa mwanga) wake, na pia ugunduzi wa kipimo halisi cha hesabu ya mwaka.

Chuo cha Baghdad kiligundua kuwa maeneo ya juu ya mwezi hayafuati kanuni maalum. Pia walitabiri kuwepo kwa vituo vya

jua, kupatwa kwa mwezi na jua na kuwepo kwa vimondo na madude mengine angani.

Walitafiti na kubaini kuwepo kwa mzunguko wa dunia kwa jua. Pia walikuwa watafiti wa kwanza kugundua Copernicus na

Kepler.

Matokeo ya tafiti mbalimbali za vituo vilivyoasisiwa na Chuo cha Baghdad yaliwekwa kumbukumbu katika Jedwali la

Unajimu lililothibitishwa, na Yahya bin Abu Mansur anaaminika kuwa muasisi na mtayarishaji wa jedwali hili.

Baadhi ya wasomi waliotokana na Chuo hicho ni pamoja na AL-Baitani, ambaye Lalande amemworodhesha kuwa ni miongoni

mwa wanajimu ishirini (20) bingwa na maarufu waliowahi kutokea duniani. Mwingine ni Abu Wefa, ambaye matokeo ya

utafiti wake yalikuwa na ubora wa zaidi ya karne kumi mbele ya ule ulio tolewa na Msomi wa Denmark aliyeitwa Tycho-

Bracho, ambaye alihusishwa na ugunduzi wa Abu Wefa kuhusu tofauti ya vipindi vya mwandamo wa mwezi.

Ali Ibn Younis, mgunduzi wa (Pendulum) timazi au mizani ya saa na vipimo vya jua, ambaye Khalif AL-Haken aliyetawala

mnamo miaka ya 990 –... , alimwekea kumbukumbu kwa kujengewa kituo cha utafiti wa anga katika

Mlima Mucaddam, anaaminika kuwa mmojawapo wa waanzilishi wa Chuo cha Cairo. Alilipitia jedwali la Hakim na

kulihakiki na kuliwekea usahihi ambao haukuwahi kufikiwa na mtu yeyote hapo nyuma.

Wakati huo huo, Hassan Ibn AL-Haitan, mnajimu mwingine na mwanahisabati wa chuo cha Cairo, alitayarisha tasnifu

(treatise) au makala yake maarufu juu ya elimu ya Nuru (optics) au uoni, iliyosaidia kuweka msingi wa kazi

iliyofanywa baadae na Roger Bacon na Kepler. Haishangazi kusikia kuwa Ibn Haitan alikuwa mtaalam wa kwanza

kupendekeza lijengwe Bwawa maarufu la Aswan nchini Misri ili kuinua kiwango cha maji ya mto Nile.

Utafiti wa Anga ulitiliwa mkazo pia na utawala wa kiislam nchini Hispania. Amir wa Cordova, Abd Al-Rahman wa pili,

alionyesha shauku na nia ya kuendeleza elimu ya sayansi hii. Kwa bahati mbaya ni tafiti ndogo tulizoweza kuzipata

kutoka Hispania ilipokuwa chini ya utawala wa kiislam. Karibu kazi zao zote ziliharibiwa kutokana na vita vya

kidini, ingawa tunaelewa kuwa kwa wakati huo, vituo vya utafiti wa anga katika miji ya Toledo na Cordova vilikuwa

maarufu. Historia imeweza kutuhifadhia majina ya baadhi ya wasomi wa Andalusia kama Maslamah AL-Mahrebi, Omar Ibn

Khaldun, Ibn Rushd (Averroes) na wengine wachache. Mtu anaweza kuhisi ubora wa kazi za Waislamu hao zilizoharibiwa

kutokana na kazi zilzotolewa baadaye na wasomi wa Kikristo waliosoma kwao na wengine waliosoma baadhi ya kazi za

Waislamu. Hivyo, inaonyesha kuwa Majedwali ya kinajimu ya Mfalme Alfonso (X) wa Kumi, yalitokana na kwa kiasi kikubwa

na kazi za wasomi wa Kiislamu.

Vita na migogoro ya ndani ambayo tangu karne ya kumi na moja vilivyozikumba nchi za Asia, viliathiri sana maisha ya

kisomi yaliyokuwa yamekwisha jengeka katka jamii ya Kiislamu. Bila shaka, vita hii ilizorotesha maendeleo ya

ustaarabu wa dunia, ingawa haviku yasimamisha kabisa. Chuo cha Baghdad kwa mfano, kilinusurika na maanguko ya

kisiasa ya Makhalifa wa Nchi za Mashariki, yaliyoisambaratisha dola ya Kiislamu.

Ubunifu wa Chuo hicho haukukoma ila uliendelea hadi katikati ya karne ya 15. Wakati huohuo, mvuto wake ulienea hadi

kuzifikia nchi za Asia ya Kati, India na hata Uchina. Mmojawapo wa wasomi wa Kiislam Abd Al-Rahman Mohammed bin

Ahmad Al-Birun aliyejenga mahusiano kati ya elimu ya Wasomi wa Shule ya Baghdad na ile ya wasomi wa Kihindi,

hakukosekana hata mara moja katika Ikulu ya Mahmud hapo Ghazna, aliyeishi mnamo miaka ya  997 – 1030 

. Mojawapo ya kazi zake nyingi ni uchapisho wa vipimo vya kijiografia vya Longitudo na Latitudo za miji mikubwa

duniani.

Sultani wa Seljuk Malik Shah aliyeishi mnamo (1072 – 1092), alikuwa msomi na mtawala aliyevutiwa na taaluma ya

unajimu. Uchunguzi alioukazania ulisababisha kufanyika kwa marekebisho yaliyosahihisha na kuiboresha kalenda, karne

kumi mbele ya marekebisho yaliyofanywa kwenye kalenda ya Kigrigori (Gregorian calender). Heshima na sifa za

marekebisho hayo yanamwendea hasa Abdur Rahman Hassan na Omar Khayyam, ambao kazi yao imewafanya kuwa watu mashuhuri

wasioweza kusahaulika duniani.

Watawala wa Kimongoli nao waliikazania elimu ya sayansi. Hulagu, mtawala aliyekuwa mkatili na ambaye ndiye

aliyeuharibu mji wa Baghdad, naye alijenga kituo cha utafiti wa anga hapo Meragah, na alimteua Nasr ed – Din Tusi

kuwa Mkurugenzi wake. Huyu alihusika na ukamilishaji wa vifaa mbalimbali vilivyokuwa vikitumika kuchunguzia anga.

Kutoka katika kituo hicho kipya, matokeo ya kazi za Chuo cha Baghdad na Cairo yalifikishwa hata Uchina ilipokuwa

chini ya utawala wa Kubilai Khan.

Lakini ilikuwa ni wakati wa utawala wa Ulug Beg, mjukuu wa Tamburlaine, ambapo unajimu wa Waislam ulipopata

mafanikio makubwa kabisa. Ulug Beg ambaye jina lake kama la baba yake Shah Ruh, linahusishwa kwa karibu sana na kazi

nzuri za usanii na harakati za ufasaha (taaluma ya fasihi) zilizoendeshwa na Timuridh; alikuwa mpenzi wa taaluma ya

unajimu. Inaaminika kuwa alikuwa mmojawapo wa wasomi wa mwisho mwisho waliotokana na Shule ya Baghdad. Kazi yake,

ambayo ilichapishwa mwaka 1437, ilitoa picha halisi juu ya maarifa ya unajimu kwa siku hizo na mwelekeo wa taaluma  hiyo kwa siku zijazo.

sehemu ya kwanza

maoni

Acha Maoni

*Mashamba alama ya asteriski ni hakika kuwa thamani.