Ahlul Bait Foundation of South Africa

Ahlul Bait Foundation of South Africa

Makala zinazohusiana

NENO LA MCHAPISHAJI TOLEO LA KISWAHILI

Kitabu kilichoko mikononi mwako, ni tarjuma ya kitabu cha Kiingereza, kwa jina la "Slavery - Islamic & Western Perspectives kilichoandikwa na Mwanachuoni mkubwa Mar hum Allamah Sayyid Sa'eed Akhtar Rizvi.

Kitabu hiki kwa ufupi kinaelezea juu ya biashara ya utumwa ilivyokuwa ikiendeshwa na wazungu hapa Afrika, waki-saidiwa na Kanisa Katoloki na Makinisa mengine yaliyofu-atia. Mwandishi kwa kutumia elimu, akili, mantiki na utafi-ti wa kina, amefichua ukweli wote uliokuwa umejificha nyuma ya biashara hii ya udhalilishaji wa binadamu. Hapa Afrika na duniani kote, watu wangali wanaamini kwamba biashara ya utumwa hapa Afrika (hususan Afrika ya Mashariki) ilianzishwa na kuendeshwa na Waraabu waki-ungwa mkono na Uislamu. Kwa hiyo mbele za watu Uislamu ulionekana kama dini isiyojali ubinadamu, iliy-owaswaga mababu zetu kama wanyama na kuwafanya watumwa kwenye nchi zao. Mwandishi anayakanusha yote haya, na kuonyesha jinsi gani Uislamu ulivyokuwa dhidi ya biashara hii ya tumwa, na ulivyofanya ili kukomesha biashara hii. Na kuonyesha jinsi gani Wazungu walivy-oing'ang'ania biashara hii, na jinsi Mapadre na Maaskofu walivyozibariki meli zilizokuwa zimebeba watumwa.

2

2UTUMWA

Tumeona tukitoe kitabu hiki kwa lugha ya Kiswahili ili kizidishe mwanga wa elimu kwa Waislamu (na wasio kuwa Waislamu) wazungumzaji wa Kiswahili, na hili likiwa ndilo lengo kubwa la Taasisi yetu ya 'AFItrah Foundation' kati-ka kuwahudumia Waislamu hususan wazungumzaji wa Kiswahili.

Tunamshukuru Ndugu yetu al-Akh Salman Shou kwa

kukubali jukumu hili la kukifanyia tarjuma kitabu hiki. Vile vile tunawashukuru wale wote walioshiriki kwa njia moja au nyingine hadi kufanikisha kuchapishwa kwa kitabu hiki.

Ni matumaini yetu kwamba kitabu hiki kitakuwa ni mwanga kwa wasomaji wetu na kuzidisha upeo wao wa elimu, na kuondokana na dhana hii potofu juu ya biashara ya utumwa.

Mchapishaji: Al-Itrah Foundation S. L. P. 1017 Dar-es-Salaam Tanzania.

3UTUMWA

UTANGULIZI WA MCHAPISHAJI KWA TOLEO LA KWANZA LA KIINGEREZA

Utumwa ni moja wapo ya maovu ambayo yamekuwepo katika jamii tangu kuwepo kwa mwanadamu hapa duniani na jitihada za wanamageuzi kujaribu kuuzuia zimeshindwa kwa karne nyingi sana. Ustaarabu wa kale haukuweza kuondoa utumwa, kwa hiyo jamii za wakati huo ziliafiki kuwa nao. Baadhi ya jamii hizo za kistaarabu ziliulea utumwa. Makanisa ya Kikristo yalishiriki katika biashara ya utumwa. Mapadri wao walizibariki meli zilizokuwa zin-abeba shehena za binadamu na waliwaonya watumwa kuwa watiifu, lakini hawakuwasihi mabwana wenye kumiliki watumwa kuwa wapole kwa shehena hizo za watu. Hivi karibuni mnamo mwaka 1970 Kanisa Katoliki lilinunua wasichana 1500 kutoka India, eti kwa sababu wasichana wa kizungu huko Ulaya hawakutaka kuishi maisha ya kitawa (usista). Miongoni mwa dini zote ni Uislamu tu ndio ulio-haribu misingi yote ya uovu huu. Lakini, ni kejeli ya histo-ria kwamba watu walio rutubisha utumwa wakasaidia uen-deleaji wake na walifaidika nao, baadaye ndio wakawa mabingwa wa kuukomesha.

Allamah Sayyid Saeed Akhtar Rizvi, Mhubiri Mkuu wa Bilal Muslim Missioni of Tanzania, amekiandika kitabu hiki kwa uwezo mkubwa na jitihada. Kama ilivyo kwa msomi mtafi-ti kama yeye, ameshuhgulikia mada ya kitabu hiki bila upen-deleo, Ameupanga ukweli baada ya ukweli kutoka kwenye historia; amenukuu kutoka kwenye Qur'ani, hadithi na waandishi wa zama za leo kuhusu somo hili, na ameonyesha sheria za Kiislamu na zile zilizotumika kabla ya Uislamu.

4

4UTUMWA

Ameonyesha waziwazi kwamba ustaarabu wa Kimagharibi sio bingwa mkubwa kiasi hicho wa kuwaokoa watumwa kama unavyojionyesha. Kwa kweli kitabu hiki kitathibitisha kuwa kifungua macho kwa wale ambao hukubali bila kuchunguza kuhusu propaganda ya ubinadamu wa Kimagharibi.

Peermahomed Ebrahim Trust kwa fahari kubwa wanakileta kitabu hiki kwa wasomaji na wana matumaini kitakubaliwa na jamii.

Wadhamini,

Peermahomed Ebrahim Trust Karachi, Pakistan

15 Jamadi, 1392

27 June, 1972.

5

5UTUMWA

UTANGULIZI WA MWANDISHI KWA TOLEO LA PILI

Kitabu hiki kiliandikwa kwa ombi la marehemu Haji Hasanali P. Ebrahim, ambaye ndiye aliye kichapisha kutoka kwa Peermahomed Ebrahim Trust, Karachi, mnamo mwaka 1972. Mara baada ya kuchapishwa, nakala zote zilinunuli-wa, lakini mahitaji yakawa bado yanaendelea. Kwa kukid-hi mahitaji hayo, mwanangu, Hujjatul Islam Sayyid Muhammad Rizvi sasa ametayarisha toleo la pili.

Baadhi ya mabadiliko madogo madogo yamefanywa katika mpangilio wa Sura; ibara zimeongezwa hapa na pale; na mwanangu ametayarisha maelezo ya ufafanuzi chini ya kurasa, ambayo yameongeza ubora wa kitaaluma wa kitabu hiki. Mwenyezi Mungu na amrefushie maisha na amwongeze nguvu za kuendelea kuutumikia Uislamu wa kweli kwa uaminifu.

Pia ninawashukuru marafiki ambao wamenisaidia kwa namna yoyote ile katika kufanikisha kuchapishwa toleo hili:

S.S. A. Rizvi Gopalpur (India) 28 Novemba 1987.

maoni

Acha Maoni

*Mashamba alama ya asteriski ni hakika kuwa thamani.