MAELEZO KWA UFUPI KUHUSIANA NA IMAM MAHDI

MAELEZO KWA UFUPI KUHUSIANA NA IMAM MAHDI

    BISMIL LAHIR RAHMANIR RAHIM
HAYA NI MAELEZO  KWA UFUPI KUHUSU IMAM MAHDI (A.S)

Imam Mahdi (a.s) ni mmoja kati ya viongozi kumi na mbili wa kiislamu waliotajwa na Mtume (s.a.w.w) naye ni kiongozi wa kumi na mbili, yaani yeye ndiye kingozi wa mwisho katika umma huu wa kiislamu.

Maimamu kumi na mbili waliotajwa na Mtume (s.a.w.w) ndio viongozi halisi wa umma huu nao wote wanatokana na kizazi cha bwana Mtume (s.a.w.w), Imamu kwa kawaida ni mtu aliebobea vyema elimu na siasa kwa ujumla na si kila mtu anaweza kua ni Imamu wa umma fulani pasi na kua na masharti maalum kati ya mashati ya Imamu ni kutokkua na makosa ya aina yeyote ile vile vile uadilifu pamoja na  elimu itokayo kwa Alla (s.w), yaani Imamu takiwi kua ameipata elimu yake vichochoroni.
Kwa hiyo basi si kila mtu aweza kudai kua yeye ni Imamu pasi na kua na masharti ya uimamu, kuna wengi walio wazushi waliodai kkua wao ni Maimamu lakini kwa kutokua na masharti hayo hawakuweza kukubalika katika jamii zao, tukiangalia Qurani vipi inasema tutagundua ukweli huu, kwani Nabii Ibraahim (a.s) alipoambiwa na Mola wake kuwa amepewa  cheo cha uimamu alikua tayari ameshapimwa kwa kupitia vipimo tofauti kikiwemo kipimo cha kuamrisha amchinje mwanawe (yaani Ismaail (a.s) naye akakubali kufanya hivyo, kwa kweli mtu wa kawaida kukubali na kkua mtiifu kiasi hicho kwa huu ni mtihani mzito aliopewa Ibraahim (a.s).    


 

maoni

Acha Maoni

*Mashamba alama ya asteriski ni hakika kuwa thamani.