DALILI ZILIZOPELEKEA UBABAISHAJI

DALILI ZILIZOPELEKEA UBABAISHAJI

Aya hizo za Mutashabih zilizoeleka katika zama za Kiarabu na kulikuwa hakuna hitilafu wala shaka zozote kuhusiana na Aya hizo, ama baada ya kuvumbuliwa madhehebu tofauti miongoni mwa watu ambayo yalipelekea hitilafu kiakida na kifikra kulivumbuliwa Aya hizo Mutashabih kutokana na rai za baadhi ya watu.

Ayatu Mutashabih zilizo asili ni za kawaida, kwa sababu kila ubabaishaji uliojitokeza katika Aya hizo ni kutokana na ubainishwaji wa maana iliyovumbuliwa kupitia maneno ambayo yamezoeleka katika jamii ya Kiarabu.


KUZIFASIRI NA KUZIBADILISHA AYA ZA QUR-ANIAya zote za Qur-ani, ikiwa Aya za Muhkamu au Mutashabih zina ugumu wake katika kuzifahamu, ama katika Ayatu Mutashabih mbali ya kuwepo ugumu huo wa kuzifahamu vile vile huleta shaka katika maana ile iliyofahamiwa, kwa sababu hiyo basi ili kuzifahamu aya za Mutashabih mwanzo kabisa ni lazima tuondowe ugumu unaopelekea kuzifahamu Aya hizo na baadae tuondowe na kuipinga shaka iliyopelekea kutofahamiwa Aya hiyo, ugumu huo unaopelekea kutozifahamu Ayatu Muhkamu na Ayatu Mutashabih huitwa Tafsiri, na ubainishwaji wa shaka ambayo huweza kujitokeza katika Ayatu Mutashabih huitwa Taawili yaani (kubadilishwa).

Wafasiri wamesema kuwa kuondowa ugumu unaopelekea kutofahamika maneno Aya za Mutashabih ni tatizo, pindi kunapokuwa na ugumu huo katika Aya ambao hupelekea kufichika maana sahihi ya Aya hiyo, Mfasiri hutumia njia ambazo ziko katika hiyari yake ili kuondowa matatizo na ugumu huo. (rejea Mabani tafsiri na nyezo za kuondowa ugumu katika kuzifasiri Aya za Qur-ani).Neno (تاویل) linatokana na neno (اول) likiwa na maana ya kurejea, kwa hiyo maana ya kilugha ya neno (تاویل) ni kurejea. (تاویل) hutumika katika maneno au mazungumzo ambayo huleta shaka na yenye kutatiza na kubabaisha, na mtu ambaye huondowa ugumu na shaka hiyo ambayo imepelekea kutofahamika maana ya maneno au Aya, kwa hiyo mtu anayejuwa kuyafasiri maneno kwa njia sahihi na huondowa shaka hiyo.

Kutokana na yale yaliyomkuta na kumstaajabisha Nabii Mussa (a.s) basi alinadi ili kupata habari, na walimpasha habari ya yale yaliyotokea, Allah (s.w) katika suratul-Kahfi Aya ya 78 anasema:-قَالَ هَذَا فِرَاقُ بَيْنِى وَبَيْنِكَ سَاُنَبِّئُكَ بِتَاْوِيلِ مَا لَمْ تَسْتَطِع عَّلَيْهِ صَبْراً(Yule mtu) akasema: "Huku ndiko kufarikiana baina ya mimi na wewe. Hivi sasa nitakwambia hakika ya yale ambayo hukuweza kuyavumilia."

Kutokana na maelezo hayo yaliyoelezewa hapo juu itafahamika kuwa kila aya yenye kubabaisha mbali na kutafsiriwa vile vile inahitajika kutafutiwa njia ambazo zinaweza zikafafanuwa kwa uwazi yale yaliyomo katika Aya hiyo yaani (تفسیر), tafsiri huondowa ule ugumu uliopelekea kutofahamika Aya hiyo, na (تاویل) huondowa shaka iliyomo katika Aya hiyo. Ama Ayatu Muhkamu yaani (Aya zilizo thabiti na zinazofahamika kwa urahisi) zinahitajia kutafsiriwa tu ili kuondowa ugumu uliopo katika Aya hiyo, kwa hiyo (تاویل) inakusanya maana ya kipekee tofauti na tafsiri, yaani kila sehemu inayokuja tafsiri na Taawili pia ipo, kwa sababu taawili ni aina moja wapo ya tafsiri.


NI NANI WANAOFAHAMU KUZIFASIRI AYA ZINAZOBABAISHA NDANI YA QUR-ANI?Katika aya ya saba ya Suratul-Al-Imrani baada ya kuzigawa Aya za Qur-ani katika sehemu mbili yaani (Muhkamu na Mutashabih) vile vile wameelezewa watu ambao wanafahamu kuzifafanuwa Aya hizo kwa njia iliyo sahihi, Allaah (s.w) katika sura hiyo ya Al-Imrani aya ya saba anaendelea kwa kusema:-هُوَ الَّذِيَ اَنزَلَ عَلَيْكَ الْكِتَابَ مِنْهُ آيَاتٌ مُّحْكَمَاتٌ هُنَّ اُمُّ الْكِتَابِ وَاُخَرُ مُتَشَابِهَاتٌ فَاَمَّا الَّذِينَ في قُلُوبِهِمْ زَيْغٌ فَيَتَّبِعُونَ مَا تَشَابَهَ مِنْهُ ابْتِغَاء الْفِتْنَةِ وَابْتِغَاء تَاْوِيلِهِ وَمَا يَعْلَمُ تَاْوِيلَهُ إِلاَّ اللّهُ وَالرَّاسِخُونَ فِى الْعِلْمِ يَقُولُونَ آمَنَّا بِهِ كُلٌّ مِّنْ عِندِ رَبِّنَا وَمَا يَذَّكَّرُ إِلاَّ اُوْلُواْ الالْبَابِYeye ndiye aliyekuteremshia Kitabu (hiki Qur-ani). Ndani yake zimo Aya Muhkamu (nyepesi kufahamika) ambazo ndizo msingi (asili) wa kitabu (hiki). Na ziko nyengine Mutashabih (zinababaisha, kama habari za Akhera, za Peponi na Motoni na mengineyo ambayo yamekhusika na Roho). Wale ambao nyoyoni mwao mna upotofu wanafuata zile zinazobabaisha kwa kutaka kuwaharibu watu na kutaka kujua hakika yake vipi, na hakuna ajuaye hakika yake vipi; ila Mwenyeezi Mungu. Na wale waliozama katika elimu husema: " Tumeziamini, zote zimetoka kwa Mola wetu." Na hawakumbuki isipokuwa wenye akili.Kutokana na maelezo yaliyoelezewa katika Aya hiyo imefahamika kuwa Aya Mutashabih vile vile zinafahamika na Maulamaa, na wanaelimu ambao ni wenye kuzifuata njia za Mwenyeezi Mungu ili kuzifahamu Aya hizo wamesema: sio Aya Muhkamu wala Mutashabih zinatokana na mwenyeezi Mungu mmoja, basi kwa hakika Aya hizo zinafahamiwa na watu wenye akili.Kutokuwepo njia ya kufikia katika uhakika wa Qur-ani ni jambo lisilokubalika kiakili, kwa sababu kama tukijaalia kuwa katika Kitabu cha Qur-ani kuna Aya ambazo hakuna mtu yoyote anayejua kuzifasiri kwa maana yake ya ndani kabisa wakiwemo Mitume Maimamu, Maulamaa, Wanaelimu na waislamu kwa jumla, itawafanya watu wajiulize masuala akilini mwao kuhusu ile hekima ya Mwenyeezi Mungu, vipi inawezekana iwe hivyo katika hali ambayo kitabu cha Qur-ani ni kitabu cha uongofu kwa kila mwanaadamu hivyo kama kutakuwa hakuna uwezekano wa mtu kufahamu au kuyatilia shaka yale yaliyomo itakuwa ni mbali na hekima ya Mwenyeezi Mungu.

Kwa hiyo kuna Maulamaa wengi wanaofahamu kwa uhakika maana za Aya Mutashabih, tukithibitisha kupitia aya ya Qur-ani Allah (s.w) anasema:-

یقولون امنا به..., Aya hiyo inathibitisha kuwa na imani thabiti watu hao katika kuziamini Aya za Mwenyeezi Mungu, watu hao wanajitahidi katika kutafuta uhakika wa Aya Mutashabih, watu hao ni wenye elimu nyingi na wasioyumbayumba katika kufafanua uhakika wa Aya Mutashabih, kwa sababu wanaelewa kwamba chanzo cha Aya Mutashabih, ndio chanzo cha Aya Muhkamu.


MIFANO YA AYA MUTASHABIHHapo nyuma tulielezea kwamba Aya Mutashabih zimegawika katika sehemu mbili, nazo ni Aya Mutashabih zilizo asili, na Aya Mutashabih zisizo asili. Katika sehemu hii tutatoa mfano kwa kila sehemu moja.1. KUKATAA KUWA MWENYEEZI MUNGU YUKO KATIKA SEHEMU FULANIMwenyeezi Mungu hawezi kufananizwa na kitu chochote kile, wala kufikiriwa kuwa yuko katika sehemu fulani, kwani tukifikiria kuwa Mwenyeezi Mungu yuko katika sehemu fulani ni lazima sehemu hiyo iwe na upande wa kulia, kushoto, mbele, nyuma, juu na chini, na hizo ni katika sifa kiumbe kilichoko katika ulimwengu wa kimada, kwa hiyo kama tukiyakubali hayo ni lazima itathibitika kuwa Mwenyeezi Mungu ana kiwili kiwili, katika hali ambayo tunaelewa kuwa Mwenyeezi Mungu hafananizwi na kitu chochote ulimwenguni.

Bwana Abul-Hassani Ash-ariy (shekhe Ash-ary) ana itikadi ya kuwa Mwenyeezi Mungu yupo katika sehemu (yaani katika arshi, yaani (mbinguni)). Na anatowa ushahidi wake kupitia Aya za Qur-ani, (rejea Kitabu Tamhiydiy, juzuu ya 3, ukurasa wa 111-113, na 115- 116), au rejea Kitabu Al-Ibanat, ukurasa wa 26-28).

Miongoni mwa Aya anazozithibitishia bwana Abul-Hassani Ash-ary juu ya kuwepo Mwenyeezi Mungu ktika sehemu ni hizi zifuatazo:-Surat Taha Aya ya 5الرَّحْمَنُ عَلـٰي الْعَرْشِ اسْتَوَي

Ndiye Mungu Mwenye rehema Aliyetawala juu ya kiti (chake) cha Enzi.

Surat sajdah Aya ya 5يُدَبِّرُ الاَمْرَ مِنَ السَّمَاءِ إِلَي الاَرْضِ ثُمَّ يَعْرُجُ إِلَيْهِ فِى يَوْمٍ كَانَ مِقْدَارُهُ اَلْفَ سَنَةٍ مِّمَّا تَعُدُّونAnapitisha mambo yote yaliyo baina mbingu na ardhi, kasha yanapanda kwake kwa siku moja tu, ambayo kipimo chake ni myaka elfu mnayotumia nyinyi katika kuhesabu kwenu.Surat Nahli Aya ya 50يَخَافُونَ رَبَّهُم مِّن فَوْقِهِمْ وَيَفْعَلُونَ مَا يُؤْمَرُونَWanamuogopa Mola wao aliye juu yao, na wanatenda wanayoamrishwa.Wafuasi wa Maktaba ya Imamiya na Muutazilah wanaitikadi ya kuwa Mwenyeezi Mungu hayuko katika sehemu maalumu, hajafanana na kitu chochote, na wanathibitisha hayo kupitia Aya ya Qur-ani ya Surat Shura Aya ya 11, Allah (s.w) anasema:-فَاطِرُ السَّمَاوَاتِ وَالاَرْضِ جَعَلَ لَكُم مِّنْ اَنفُسِكُمْ اَزْوَاجاً وَمِنَ الاَنْعَامِ اَزْوَاجاً يَذْرَؤُكُمْ فِيهِ لَيْسَ كَمِثْلِهِ شَيْءٌ وَهُوَ السَّمِيعُ البَصِيرُ(Yeye ndiye) muumba wa mbingu na ardhi. Amekuumbieni wake (zenu) katika jinsi yenu; na wanyama nao (akawaumbia) wake (zao katika jinsi moja na wao); anakuzidisheni kwa namna hii (ya kuchanganyika kwa dume na jike). Hakuna chochote mfano Wake; naye ni Mwenye kusikia, Mwenye kuona.Imamiya na Muutazilah wanaitikadi ya kuwa Aya hiyo ni katika Aya Muhkamu, ama wafuasi wa maktaba ya Ash-ary wana nadharia ya kuwa Aya hiyo ya 11 ya Surat Shura ni katika Aya Mutashabih, wafuasi wa maktaba ya Ash-ary wameifasiri Aya hiyo kwa kuibadilisha, yaani wanasema kwamba Mwenyeezi Mungu yupo katika sehemu – na kama tukijaalia hivyo basi hakuna shaka ni sehemu iliyo juu na bora kabisa duniani, na baraka zote za ulimwenguni ni zake, na matendo ya amali njema yaliyofanywa na watu wema yanamfikia yeye, kwa hiyo Mwenyeezi Mungu atakuwa yupo katika sehemu maalumu. Katika Aya ya 115 ya suratul-Baqara Allah (s.w)anasema:-وَلِلّهِ الْمَشْرِقُ وَالْمَغْرِبُ فَاَيْنَمَا تُوَلُّواْ فَثَمَّ وَجْهُ اللهِ إِنَّ اللّهَ وَاسِعٌ عَلِيمٌNa Mashariki na Magharibi ni ya Mwenyeezi Mungu. Basi mahala popote mgeukiapo (alikokuamrisheni Mwenyeezi Mungu mtazikuta) huko radhi za Mwenyeezi Mungu. Bila shaka Mwenyeezi Mungu ni Mwenye wasaa (mkubwa kabisa) na Mwenye kujua (kukubwa kabisa vile vile).Aya ambazo wamezitumia wafuasi wa madhehebu ya Ash-ary katika kuthibitisha nadharia yao hiyo ni katika Aya Muhkamu, na waislamu walikuwa wakifahamu kwa uhakika maana ya Aya hizo, ama baada ya kupita muda wafuasi wa maktaba ya Ash-ary ili kutilia debe maktaba yao walizitumia Aya hizo kuzibadilisha na kuzifasiri na vile wanavyotaka wenyewe, na kudai kuwa Aya hizo ni katika Aya Mutashabih, na kwa sababu hiyo basi Aya hizo huitwa Aya Mutashabih zisizo asili.2. MATENDO YOTE ANAYOYAFANYA MWANAADAMU ANAYAFANYA KWA HIYARI YAKE.Hapo mwanzo tulifafanua Aya Mutashabih zilizo asili na tulielezea kwa kusema kuwa chanzo cha Aya hizo ni kuwepo kwa maana refu na pana iliyotokana na maneno mafupi, moja katika Aya ambazo zina sifa kama hizo ni Aya ya 17 ya Suratul-Anfal, Allah (s.w) anasema:-فَلَمْ تَقْتُلُوهُمْ وَلَـكِنَّ اللّهَ قَتَلَهُمْ وَمَا رَمَيْتَ إِذْ رَمَيْتَ وَلَـكِنَّ اللّهَ رَمَي وَلِيُبْلِيَ الْمُؤْمِنِينَ مِنْهُ بَلاء حَسَناً إِنَّ اللّهَ سَمِيعٌ عَلِيمٌHamkuwauwa nyinyi lakini Mwenyeezi Mungu ndiye aliyewauwa; na hukutupa wewe (Mtume ule mchanga wa katika gao la mkono wako), ulipotupa (ukawaingia wote machoni mwao); (hukufanya wewe haya) walakini Mwenyeezi Mungu ndiye aliyeutupa, (yaani ndiye aliyeufikisha katika macho yao wote yakawa yanawawasha kuliko pili pili wakenda mbio) Aliyafanya haya Mwenyeezi Mungu ili awape walioamini hidaya nzuri itokayo kwake. Hakika Mwenyeezi Mungu ndiye asikiaye na ajuaye.

Katika zama za kale zilizopita watu wa jamii ya Kiarabu waliifahamu Aya hiyo kuwa ni yenye kuthibitisha kulazimika kwa mwanaadamu kufanya matendo tofauti, - yaani kila analolifanya mwanaadamu halifanyi kwa hiyari yake – katika hali ambayo Aya hiyo inamaanisha uwezo mdogo alionao mwanaadamu ndio dalili moja wapo inayomfanya awe na hiyari katika kufanya matendo yake ambayo anayafanya kutokana na idhini ya Mola wake, zama hizo ilikuwa ni vigumu sana watu kufahamu maana ya Aya hiyo, kwa hiyo basi ndiyo ikaitwa Aya Mutashabih iliyo asili.

maoni

Acha Maoni

*Mashamba alama ya asteriski ni hakika kuwa thamani.