SEHEMU YA PILI MAHDI NI NANI ?

SEHEMU   YA  PILI     MAHDI  NI  NANI ?SEHEMU YA PILIMAHDI NI NANI ?Hakika Uislamu uliipinga rai ya mayahudi ya kuwa “Elia” ndie msuluhishaji mwenye kusubiriwa na pia rai ya wakristo isemayo kuwa yeye ni “Issa mwana wa Maryam”.Vilevile hali ya wazi ya matokeo ya nje imeipinga rai ya madhehebu ya kiisaaniya ya kuwa huyo mwenye kusubiriwa ni “Muhammadi bin Alhanafiya” na madhehebu ya “Ismaailiyya, ya kuwa huyo ni “Ismaail bin Jaafar” kwani imethibiti kufariki kwa Muhammad na Ismaili na kubatilika fikra ya kubakia kwao. Basi imebaki tofauti na hitilafu kati ya Ahli sunna na Shia Imamiya katika kumuainisha Mahdi ni nani.

Na muhtasari wa itikadi za Ahli sunna ni kuwa Mahdi atadhihiri zama za mwisho na atasimama kwa upanga na kwamba “Habari zake zimekuwa mutawaatiri (nyingi sana na zingine mustafidhi, kwenye kila tabaka kuna wapokezi wawili au watatu” kwa wingi wa wapokezi wake kutoka kwa Mtume (s.a.w) kuhusu kutokea kwake na kwamba yeye anatokana na kizazi chake Mtume, na kwamba atamiliki au kutawala kwa muda wa miaka saba.

Na kwamba ataijaza ardhi na ulimwengu kwa uadilifu, na kwamba atatoka pamoja na Issa (a.s) na kuwa yeye atawaongoza kwenye sala umma huu na Issa atasali nyuma yake.[28]

Na muhtasari wa itikadi ya Shia Imamiyya ni kuwa atadhi-hiri katika zama za mwisho Mahdi atokanae na nasaba ya Ali na atasimama kwa upanga, na kwamba ataujaza ulimwengu uadilifu na usawa na atatengeneza mazingira yawezeshayo kuutekeleza Uislamu kiukamilifu katika ardhi yote.

Kwa hivyo ni sehemu ipi yenye tofauti kati ya kauli mbili hizi?

Hakika kati yao imefungika kwa upande wa masunni kwenye kauli au kwenye itikadi yao ya kuwa, Mahdi huyu atazaliwa katika zama za mwisho, na hivi sasa hayupo, na haijulikani ni wakati gani atakao zaliwa na baba yake ni nani? Kwa msingi huu aliweza Sunuusiy huko Libia na Abdul-Rahmaan wa huko Sudan na wengineo kudai kuwa wao ni akina Mahdi na kusimama kwa upanga (Silaha).

Ama Shia Imamiyya, wao rai yao ni kuwa Mahdi ni Muhammad bin Hassan bin Ali bin Muhammad bin Ali bin Mussa bin Jaafar bin Muhammad bin Ali bin Hussen bin Ali bin Abi twaalib (a.s) na kwamba yupo kwenye dunia hii lakini watu hawamtambui. Na hii ndio nukta yenye tofauti kati ya pande hizi mbili.

Kutokana na ukweli kuwa mwenye kutoa madai ndio huiti-shwa dalili ya madai yake, kama ilivyo katika fiqhi (sharia) ya kiislamu, basi sisi tutatoa ushahidi ambao wana utegemea Mashia kwenye kuthibitisha yale wanayo yaitakidi, na tutaonyesha usha-hidi mwingine walio utumia kuzibatilisha rai za wapingao fikra hii, ili jambo hili liweze kuonekana na kujulikana wazi kwa kila mwenye macho mawili. Na kutokana na ukweli kuwa mashia kama tulivyo eleza mwanzoni mwa maudhui haya kuwa wana amini kuwa uimamu ni cheo cha kupewa na Mwenyezi Mungu na kina hitajia dalili na uteuzi, wame amini kuwa uimamu wa Mahdi, Muhammad bin Hassan kufuatana na dalili zilizopo na kwa kuzitii dalili hizo, na kufuatana na matamshi yake yaliyo wazi kabisa.

Huenda kukawa na mwenye kuuliza, dalili hizo ni zipi na lafdhi zake ni zipi na ni nani alie zisimulia na kuzipokea?

Ili kulifafanua jawabu la swali hilo ni lazima kuashiria kuwa dalili hizo zimhusuzo Mahdi haikuwa ni habari ( hadithi) moja au mbili, bali ni habari nyingi zilizotoka kwa Mtume (s.a.w) na zilizo mutawaatir zilizovuka mamia, na zilipokewa na idadi kubwa ya maswahaba, na zikatolewa na idadi kubwa nyingine ya mahuffa-dhi na wapokezi, na kwa wingi wa istifadha (wapokezi watatu kwenye kila tabaka) tawaatur (wapokezi wengi sana) haikuwa tena ni sahihi kufanya mjadala kuhusu usahihi wa hadithi hizi na kuhusu yakini zinazo tuletea katika kuthibitisha swala hilo. Na kwa ajili ya udadisi zaidi na utafiti wa kimaudhui tunasema:

Hakika hadithi hizi kwa sanadi yake na dalili yake zimegawa-nyika kwenye makundi matatu:

Kundi la kwanza:

Zenye sanadi sahihi na dalili yake ni ya dhahiri zisizo na shaka yoyote, na maimamu wa hadithi na mahufadhi wakubwa walithibitisha juu ya usahihi wake au kuwa ni hassan[29](nzuri) na kuwa baadhi yake ni sahihi kufuatana na masharti ya mashekh wawili, Bukhari na Muslim.

Na hakuna shaka katika uwajibu wa kuzichukuwa hadithi za kundi hili na kuzifanyia kazi na kuyaamini mambo yanayo zungumziwa na kujulishwa na hadithi hizo.Kundi la pili:

Ni hadithi zisizo sahihi katika sanadi yake hata kama dalili yake (yaani maneno yake) iko dhahiri. Kanuni zilizo kubaliwa kwenye elimu ya hadithi zinatulazimisha kuzichukua hadithi hizo vilevile, kwa kuungana kwake na kusahihishwa kwake na kundi la kwanza na kwa kuwa mashuhuri ya kuwa wanazuoni wame-zikubali, bali wanazuoni wote wamefanya ijmai kuafikiana juu ya madhumuni yake.Na kundi la tatu:

Limekusanya sahihi na dhaifu, lakini hadithi hizo zinapi-ngana na hadithi zingine zote ambazo ni mustafidhi na zilizo mutawaatir. Basi kitu cha lazima ni kuziacha, na kujiepusha nazo, ikiwa haikuwezekana kuzifanyia ta’awili, kwa mfano zilizosema kuwa jina la Mahdi ni Ahmad au zilizo sema kuwa jina la baba yake linafanana na jina la baba yake mtume (s.a.w) au zisemazo kuwa yeye anatokana na watoto wa Abi Muhammad Hassan Az-Zakiy, kwani habari hizi ni habari chache na nadra ambazo wanazuoni mashuhuri wamejiepusha nazo.[30]

Hadithi za makundi mawili la kwanza na la pili hizo ndizo ambazo tumebainisha kuwa ni wajibu kuzichukuwa zilikuwa zikielekeza kwenye lengo kwa ibara tofauti tofauti na zikikusudia kumtambulisha na kumuainisha kwa matamshi tofauti tofauti na tunaweza kuufupisha muhtasari wake kama ifuatavyo:

Baadhi ya hadithi hizo zimethibitisha kuwa Mahdi anatokana na kabila la kikuraishi. Ametoa Ahmad na Al-manwardi ya kuwa Mtume (s.a.w) amesema:

)ابشروا بالمهدي،رجل من قريش،من عترتي،يخرج في اختلاف من النَاس و زلزال،فيملأ الأرض عدلاً وقسطاً كما ملئت ظلماً و جوراً(

“Pateni bishara ya Mahdi, ni mtu atokae kwenye kabila la kuraishi, atokae kwenye kizazi changu. Atatoka watu watakapo hitilafiana na kuwepo mtetemeko, na kuijaza ardhi kwa uadilifu na usawa kama ilivyo jazwa dhuluma na ujeuri”.[31]

Na zingine zimethibitisha, kuwa Mahdi ni katika watoto wa Abdul-Mutwalib.

Ametoa Ibn Maaja kwa sanadi yake kutoka kwa Anas bin Maalik, amesema: Nilimsikia Mtume (s.a.w) akisema:

نحن ولد عبد المطلب سادة اهل الجنَة:انا و حمزة وعلي وجعفر والحسن والحسين ) ( والمهدي

“Sisi watoto wa Abdul-Mutwalib ni mabwana wa watu wa peponi, Mimi na Hamza na Ali na Ja’afar na Hassan na Hussen na Mahdi”.[32]

Na zingine zimethibitisha kuwa yeye ni katika Aalu Muhammad (Kizazi cha Mtume,(s.a.w). Amesema Mtume (s.a.w):

يخرج في آخر الزمان رجل من ولدي ،إسمه كإسمي،وكنيته ككنيتي،يملأ الأرض) ( عدلاً كما ملئت جوراً،فذلك هو المهدي “Atatoka katika Zama za mwisho mtu atokanae na kizazi changu, jina lake ni kama jina langu, na kuniya yake ni kama yangu (jina la ubaba kwa mfano baba ya fulani) ataijaza ardhi kwa uadilifu kama ilivyo jazwa ujeuri, na huyo ndie Mahdi”. Na hii ni hadithi mashuhuri.[33]

Na zingine zimethibitisha kuwa ni katika kizazi chake. Ametoa Abu Daud kwa Sanadi yake kutoka kwa Ummu Salama (Mungu amuwie radhi) amesema:“Nilimsikia Mtume (s.a.w) akisema:

“( من عترتي المهدي) Madhi anatoka katika kizazi changu”.[34]

Na zingine zimethibitisha kuwa yeye ni katika Ahlul bayti. Amesema Mtume (s.a.w):

(لولم يبق من الدهر إلاً يوم لبعث الله رجلاً من اهل بيتي،يملأها عدلاً كما ملئت جورا)

“Lau kama isingebakia isipokuwa siku moja Mwenyezi Mungu angetuma mtu atokanae na Ahlul-bayti wangu aujaze ulimwengu uadilifu kama ulivyo jazwa ujeuri.[35]

Na zingine zimethibitisha kuwa, anatokana na watoto wa Ali (a.s), kutoka kwa Said bin Jubair kutoka kwa Ibnu Abbas (Mungu awawie radhi) amesema: “Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu:

)ان علياً وصيي،ومن ولده القائم المنتظر المهدي الذي يملأ الأرض قسطاً وعدلاً كما ملئت جوراً و ظلماً(.

“Hakika Ali (a.s) ni wasii wangu na katika kizazi chake atatoka huyo mwenye kusimama (dhidi ya dhulma) na mwenye kusubiriwa (almuntadhar), ambae ni Mahdi atakae ijaza ardhi usawa na uadilifu kama ulvyo jazwa ujeuri na dhulma”.[36]

Na zingine zimethibitisha kuwa ni katika watoto wa Fatima.

Ametoa Muslim na Abu daud na Nasai na Ibnu Maaja na Bayhaqiy na wengine:

(المهدي من عترتي من ولد فاطمة) “Mahdi ni katika kizazi changu ni katika watoto wa Fatuma”.[37]

Na wengine wamethibitisha kuwa ni katika watoto wa Hussen, Amesema Mtume (s.a.w):

)لا تذهب الدنيا حتى يقوم بأمتي رجل من ولد الحسين يملأ الأرض عدلاً كما ملئت ظلماً(

“Haitaondoka dunia mpaka ausimamie umma wangu mtu atokanae na kizazi cha Hussen, aijaze ardhi kwa uadilifu kama ilivyo jazwa dhulma”.[38]

Na zingine zimethibitisha kuwa ni wa tisa katika kizazi cha Hussen. Kutoka kwa Salmani Al-faarisi (Mungu amuwie radhi) amesema:“Niliingia nyumbani kwa Mtume (s.a.w) mara nika-muona Hussen akiwa mapajani mwake akilibusu shavu lake na kuulamba mdomo wake na akisema:

)انت سيد ابن سيد اخوسيد،وانت امام ابن امام اخو امام،وانت حجة ابن حجة اخو حجة ابو الحجج تسعة تاسعهم قائمهم المهدي(.

“Wewe ni Sayyid mtoto wa Sayyid, nduguye Sayyid, na wewe ni Imam Mtoto wa Imam na ndugu wa Imamu, na wewe ni Hujja mtoto wa Hujja ndugu wa Hujja baba wa Mahujja tisa, wa tisa wao ni yule atakae simama (dhidi ya dhulma) ambae ni Mahdi.[39]

Na zingine zilithibitisha kuwa yeye ni wasii wa kumi na mbili. Na Imamu wa kumi na mbili na khalifa wa kumi na mbili.

)ان وصيي علي بن ابي طالب و بعده سبطان الحسن والحسين تتلوه تسعة أئمة من صلب الحسين،قال يا محمَد فسمهم لي،قال:اذا مضى الحسين فإبنه علي،فإذا مضى علي فإبنه محمَد فإذا مضى محمَد فإبنه جعفر فإذا مضى جعفر فإبنه موسى،فإذا مضى موسى فإبنه علي،فإذا مضى علي فإبنه محمَد فإذا مضى محمد فإبنه علي فإذا مضى علي فإبنه الحسن فإذا مضى الحسن فإبنه الحجَة محمَد المهدي فهؤلاء اثنا عشر(.

“Hakika wasii wangu ni Ali bin Abi twalib na baada yake ni wajukuu wangu wawili Hassan na Hussen watafuatiwa na maimamu tisa watokao kwenye uti wa mgongo wa Hussen (a.s), akasema:“Ewe Muhammad nitajie majina yao”. !Akasema:“Aki-ondoka Hussen ni mwanae Ali akiondoka Ali ni mwanae Muhammad, akiondoka Muhammad ni mwanae Jaafar, akiondo-ka Jaafar ni mwanae Mussa, akiondoka Mussa ni mwanae Ali, akiondoka Ali ni mwanae Muhammad, akiondoka Muhammad ni mwanae Ali akiondoka Ali ni mwanae Hassan, akiondoka Hassan ni mwanae Alhujja Muhammad Al-mahdi hawa ndio maimamu kumi na mbili”.

Yahya binil Hassan ametaja kwenye kitabu Al-umda kupitia njia ishirini za upokezi ya kwamba makhalifa baada ya Mtume (s.a.w) ni kumi na mbili na wote wanatokana na kabila la kikuraishi, katika Bukhari kupitia njia tatu za wapokezi, na katika Muslim kupitia njia tisa na kwa Abi Daud kupitia njia tatu, na katika Tirmidhi kupitia njia moja na katika Al-hamiidi kupitia njia tatu”.[40]

Na zingine zimethibitisha kuwa ni mtoto wa Hassan Al-askari.

Katika manaaqib kutoka kwa Jaabir bin Abdillahi al-answary kutoka kwa Mtume (s.a.w):

)...فبعده ابنه الحسن يدعى بالعسكري،فبعده ابنه محمَد يدعى بالمهدي و القائم والحجَة،فيغيب ثمَ يخرج، فإذا خرج يملأ الأرض قسطاً وعدلاً كما ملئت جوراً وظلماً.(

“…Basi baada yake ni mwanae Hassan aitwae Al-askari, na baada yake ni mwanae Muhammad aitwae Mahdi na mwenye kusimama kwa haki (Al-Qaaim) na Al-hujja, atatoweka na kutoonekana kisha atatokea, na atakapotokea ataijaza ardhi usawa na uadilifu kama ulivyo jazwa ujeuri na dhuluma.[41]

Na hivyo hivyo tunakuta kuwa hadithi hizi kwa wingi huu na tofauti zake zimemuelezea Mahdi wa umma huu, na kusema kuwa ni mtoto wa Hassan Al-askari, nayo ni matokeo au natija thabiti ambayo haina kasoro ndani yake.

Na msomaji ili awe na ujuzi zaidi wa jambo hili tunatoa katika sehemu ifuatayo majina ya wapokezi wa hadithi za Mahdi zilizotajwa hapo kabla na hasa majina ya maswahaba, kwani utafiti wetu huu wa haraka hauna nafasi kubwa ya kuweza kuandika majina ya wapokezi wote kutoka kwenye matabaka mengine:

01- Abu Amama al-baahily

02- Abu Ayyub

03- Abu Said Al khudri.

04- Abu Sulaiman-mchungaji mifugo wa Mtume (s.a.w)

05- Abu tufail.

06- Abu Huraira.

07- Ummu Habiba mama wa waumini.

08- Ummu Salama mama wa waumini

09- Anas bin Maaliki.

10- Thubaan-mtumwa wa Mtume (s.a.w).

11- Jaabir bin Samrah.

12- Jaabir bin Abdillahi al-Answari.

13- Hudhaifa binil Yamaan.

14- Salman Al-faarisi.

15- Shahr bin Hawhab.

16- Twalha bin Ubaidullah.

17- Aisha mama wa waumini.

18- Abdur-rahmaan bin Auf

19- Abdallah bin Haarith bin Hamzah.

20- Abdallah bin Abbas.

21- Abdallah bin Omar.

22- Abdallah bin Amrubinil Asi.

23- Abdallah bin Masoud.

24- Othmani bin Affan.

25- Ali bin Abitwalib.

26- Ali Alhilaali.

27- Ammar bin Yaasir.

28- Umraan bin Haswiin.

29- Auf bin Maalik.

30- Qurrat bin Iyaas.

31- Mujmau bin Jariyah Al-answari.[42]Ama ambao walitoa hadithi kuhusu Mahdi kati ya mahufadhi wa hadithi na wenye vitabu vya sahihi na sunanu, ni shekh Abdul-Muhsin Alubad aliwahesabu na kufikia “38” ambao ni mashuhuri na walio wema[43], na miongoni mwao ni:01- Abu Daud katika Sunani yake.

02- At-tirmidhi kwenye kitabu chake kiitwacho “Jami’u”.

03- Ibnu Maaja kwenye Sunani yake.

04- An-nasai kwenye kitabu chake Alkubra.

05- Ahmad kwenye Musnadi wake.

06- Ibnu Habban kwenye Swahihi yake.

07- Al-haakim kwenye Mustadrak.

08- Abubakar bin Abi Shaiba kwenye “Al-munswif”.

09- Naim bin Hamad kwenye Kitabu Al-fitani.

10- Abu Naiim kwenye kitabu “Al-Mahdi wal-hilyah”.

11- At-twabaraniy kwenye kitabu “Al-kabiir wal-awsat wa As-swaghiir.

12- Ad-daru-qutni kwenye kitabu “Al-ifrad”.

13- Al-baarudy kwenye kitabu “Ma’arifat As-swahaba”.

14-Abu Ya’ala al-muuswiliy kwenye Musnad yake.

15- Al-bazzar kwenye Musnad yake.

16- Al-haarith bin Abi Usamah kwenye Musnad yake.

17- Al-khatib kwenye kitabu chake”At-talkhisul-mutashabih” na katika “Almut- tafaq wal-muftaraq”.

18- Ibnu Asakir kwenye kitabu cha historia.

19- Ibnu Mundih kwenye kitabu chake cha historia “Taarikh Isbahan”.

20- Abul-hassan Al-harbiy kwenye kitabu chake “Al-awwal minal-harbiyaati”.

21- Tamam Ar-raziy kwenye “Fawaid”.

22- Ibnu Jariri kwenye “Tahdhibul-Athar”.

23- Abubakari bin Al-muqri kwenye “Mu’ujam” wake.

24- Abu Amru Addani kwenye Sunani yake.

25- Abu Gharam Al-kuufiy kwenye kitabu chake “Al-fitani”.

26- Ad-daylamiy kwenye kitabu chake “Musnadul-fir dausi”.

27- Abu Bakar Al-Iskaf kwenye “Fawaidul Akhbaar”.

28- Abul-Hussen binil Munawiy kwenye kitabu chake “Al- malaahim”.

29- Albaihaqi kwenye “Dalailu An-nubuwah”.

30- Abu-Amru Al-muqri, kwenye Sunani yake.

31- Ibnul Jawzi kwenye kitabu chake cha Historia.

32-Yahya Al-hamaniy kwenye Musnad wake.

33- Ar-ruyaaniy kwenye musnad wake.

34- Ibnu Sa’ad kwenye “Twabaqaat”.

Imam (Rehma za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake) alizaliwa kwenye mji wa Samarra wakati wa Al-fajiri tarehe kumi na tano ya mwezi wa Sha’aban mwaka 255H.[44] na baba yake akamuita Muhammad, na huo ulikuwa ni uthibitisho wa hadithi ya Mtume (s.a.w) iliyo maarufu isemayo “Jina lake ni sawa na jina langu”[45] na Kuniyah yake (Jina lake la ubaba) akumuita Abul-Qaasim.[46]

Na wapokezi wa riwaya wa Shia Imamiyya walisalim amri juu ya ukweli huu na wengine wengi wa makundi mengine ya kiislamu. Lakini baadhi ya waislamu pamoja na kuikubali kwao fikra ya kuja mahdi walimkataa Mahdi kwa hoja ya kuwa hakuna mtoto wa Askari, na wakatoa dalili nne kuthibitisha hoja hiyo, na tutazielezea kwa ufupi, kama ifuatavyo:

1- Walisema kuwa Askari alipo karibia kufa alimuweka mama yake (Umul-Hassan) kuwa ndie muusiwa wake wa kuya-angalia yote aliyo kuwa akiyasimamia kama vitu vya wakfu na sadaka na mambo mbali mbali mengine, kama angekuwa na mtoto asingemuacha kumuusia na kumuusia mtu mwingine.

2- Ni kuwa Jaafar bin Ali ami yake Mahdi alipinga kuwepo mtoto wa kaka yake, na ushahidi wa baba mdogo kwenye jambo kama hili ni wenye umuhimu mkubwa.

3- Hakika mashia wanadai kuwa Askari alificha suala la mwanae kwa watu wasio maalumu na wasio wa karibu, kwa nini alifanya hivyo pamoja na kuwa maswahaba wake walikuwa ni wengi katika siku hizo huku wakiwa na nguvu, mali na uwezo wakati ambapo maimamu walio tangulia kwenye zama za utawala wa bani umaya na bani Abbas walikuwa kwenye hali ngumu zaidi na wali banwa zaidi, pamoja na hayo hawakuficha suala la watoto wao kama ufichaji huu.

4- Hakika vitabu vya historia havikumfahamu na kumuelezea mtoto wa Hassan Al-Askari wala havikusimulia habari yake yoyote. Na kwa dalili hizi nne wakapinga wapingaji kuzaliwa kwa Imam Muhammad binil-Hassan.

Tutatowa sehemu ifuatayo kwa ufupi jawabu la dalili hizi ili jambo hili liweze kuwa wazi na iweze haki kudhihiri, na kwa hivyo tunasema:

Ama jawabu la dalili ya kwanza ni kuwa:

Hakika kumuusia mama haifai kuwa ni dalili ya kupinga kuwepo kwa mtoto, na lengo la Imam kutoa usia huo ni kuwafa-nya watu wasimuelekee na kutaka kujua habari za mwanawe na watu kutojishughulisha nae na mazingira kugubikwa na suala lake na kuwajulisha maadui zake kutokuwepo mwanae, bali aliwazidishia dhana hiyo kwa kuwafanya kuwa mashahidi wa Usia huo watu wengi katika wakubwa wa serikali ya wakati huo juu ya usia huu.[47]

Na Imam alikuwa kwenye matendo yake hayo akifuata mfumo wa babu yake Jaafar bin Muhammad As-swadiq (a.s) pale alipojiwekea wausiwa watano baada ya kufariki kwake nao ni Al-mansuril Abbasi na Arrabi’u na Kadhi wa madina ukiongezea mkewe Hamidah, na mwanae Mussa bin Jaafar (a.s) na lengo lake kwa kufanya hivyo ni kuyaweka mbali macho ya watawala na maadui yasimuelekee mwanae Mussa[48], kwa sababu lau kama angemuusia yeye peke yake, bani Abbasi wangeweza kufanya jambo lolote lingine tangu siku ya kufariki baba yake, na Mansur alipofikiwa na habari za kufariki Imamu Swadiq (a.s) alimuandi-kia gavana wake wa Madina, akimuamuru azidi kumbana wasii wa Jaafar bin Muhammad, yule gavana akamuandikia Mansuur, baada ya kufanya uchunguzi, akimfahamisha kuwa walio usiwa ni watu watano na kuwa wa mwanzo wao na ambae ni muhimu ni khalifa mwenyewe. Na kwa kufanya hivyo ilikuwa ni kumuepu-shia Imamu Mussa bina Jaafar (a.s) maudhi.

Ama jawabu la dalili ya pili ni kuwa:

Hakika Jaafar ni katika watu wa kawaida, na inawezekana kwake kufanya mambo kama wafanyavyo watu wengine wa kawaida kama kukosea na kuasi na kutoa madai ya batili, na inatosha akawa kama mfano wa Kaabiil, pindi alipomuua ndugu-ye au mfano wa watoto wa Yaakub walipomtumbukiza ndugu yao kwenye kisima na wakamuudhi baba yao na kuapa viapo vya uongo ya kuwa ndugu yao ameliwa na mbwa mwitu.

Na Jaafar alidhania, nae akifahamu kufichwa suala la mtoto wa kaka yake kwa watu wasio maalumu kati ya maswahaba wa baba yake, ya kuwa atakuwa Imamu kwa kupinga kule, na kwa-mba mali za kisheria zitakusanywa kwake kutoka kila pembe na kila upande, lakini Irada ya Mwenyezi Mungu ndio yenye kushi-nda, kwani ni haraka sana ulidhihiri uongo na ubaya wa suala lake, kisha akajuta kwa yale aliyoyafanya na akatubia kutokana na uovu alio ufanya hadi kuwa mashuhuri kwa jina la “ Ja’afar Attawaab”. (Mwenye kutubia)

Na si jambo la ajabu baba mdogo kusimama kidete dhidi ya mtoto wa nduguye. Hapo zamani Abu Lahab na Abbas walikuwa ni viongozi wa kikundi cha maadui dhidi ya mtoto wa ndugu yao, Muhammad (s.a.w) kwani walipinga utume wake na kumuhusisha na uchawi na wendawazimu na kuyaongoza majeshi kumpiga vita na wakaweka mipango na mikakati ya kumua.

Ama jawabu la dalili ya tatu ni kuwa:

Hakika jambo lililo mfanya Imamu Askari kuficha suala la mwanae ni kutokana na kufahamika na kuwa mashuhuri ya kuwa Imam atasimama kwa upanga ili kuondoa dola la batili na kusi-mamisha dola la haki, kwa hivyo watawala walikuwa wakimu-ogopa mwana mapinduzi huyo na wakijiandaa na kuandaa mipango ya kumuua kwa aina yoyote ile, lau wangefahamu suala lake na kujua habari zake. Kutokana na hali hii akalazimika Imam Askari kuficha na kutozisema habari za mwanae na kuzihi-fadhi habari zake kwa siri kwa maswahaba wake maalumu. Na jambo linaloweka wazi na kuyaunga mkono maneno haya ni kuwa serikali tawala za wakati huo waliharakisha kuwatuma wapelelezi wao wakati wa kufariki Imam Askari kwenye nyumba yake ili wamkamate mtoto yoyote atakae kuwa ndani ya nyumba hiyo.[49] Lau kama si utashi wa Mwenyezi Mungu ambao ulimfanyia wepesi Muhammad bin Hassan kukimbia na kujificha, wange-muua.

Na Imamu Askari katika ufichaji huu alikuwa na kigezo cha mama yake Mussa bin Imran alipo shushiwa wahyi kuwa ni lazima kumficha na kufanya siri kuhusu suala la Nabii Mussa kwa kumkhofia Fir’auni wa zama zake kama Qur’an tukufu ilivyoelezea kuhusu swala hilo.

Ama maimamu walio tangulia ilikuwa si lazima kwao kusimama kwa upanga, bali suala hilo liliachiwa kulingana na mazingira na mambo ya zama hizo na kufanya kulingana na mahitajio ya kila zama na mazingira yake kwa kujua ni hukumu gani au taklifu ipi inatakiwa, kwa hivyo walikuwa na amani kiasi na uhuru kwa kiwango fulani, hata kama haikuwa ni amani na uhuru kwa maana yake sahihi.

Ama jawabu la dalili ya nne ni kuwa:

Hakika kujulikana utoto au mtoto huyu kuwa ni wa huyu huthibitika katika sheria, kwa kauli ya mkunga au wanawake ambao huwepo kwenye uzazi ule (yaani mama yule anapo jifungua) na kwa kukubali mwenye kitanda (baba mzazi) na kushuhudia wanaume wawili walio waislam juu ya kukiri na kumkubali baba mtoto wake. Na pande hizi tatu zilithibitika na kupatikana kwenye uzazi ule.

Kwa mfano, Sayyida Hakimah binti wa Imam Jawaad (a.s) ndie ambae alisimamia jambo hilo la uzazi na akashuhudia uzazi huo. Na Imam Askari ndie baba na alikubali kuzaliwa kwa mtoto huyo mbele ya maswahaba wake maalumu.[50]

Na waislamu wa zama hadi zama zinginezo zilizo fuatia, wanasimulia habari hizo na wanashuhudia juu ya usahihi wake. Na miongoni mwa waliopokea na kusimulia uzazi huu, ukiongezea juu ya kukubaliana mashia Imamiyya wote juu ya suala hili kati ya wanazuoni wa kiislamu, kuna idadi isiyo chache ya wana historia na waandishi, kwa mfano kuna hawa wafuatao:

01-Muhammad bin Twalha Ashaafii,aliefariki mwaka 652 H.[51]

02- Sibti ibn Jawziy, aliefariki mwaka 554 H.[52]

03- Al-kanji Ashaafi’i , aliefariki mwaka 658 H.[53]

04- Ibnu Khalakaan Ashafi’i, aliefariki mwaka 681 H.[54]

05- Swalahud-dini As-swafadi aliefariki mwaka 764 H.[55]

06- Ibnu Hajar Al-haytami Ashaafi’i aliefariki mwaka 852 H.[56]

07- Ibnu Swabbagh Al-maaliki, aliefariki mwaka 855 H.[57]

08- Ibnu Tuuluum Ad-damashqi, aliefariki mwaka 953[58]

09- Al-Hussen bin Abdallah Assamar qandi, aliefariki mwaka 1043.[59]

10-Mohammad As-swaban Ashaafi’i, aliefariki mwaka 1206.[60]

11- Sulaimani Al-kanduzi’ii, Al-hanafiy aliefariki mwaka 129 H.[61]

12- Mohammad Amin As-suwaydi aliefariki mwaka 1246 H.[62]

13- Mu’umin Ashablanji Ashaafi’i, aliefariki katika karne ya 14 H.[63]

maoni

Acha Maoni

*Mashamba alama ya asteriski ni hakika kuwa thamani.