SEHEMU YA PILI

SEHEMU YA PILIMapinduzi ya Kiislam ya Iran, yaliyoweka utawala wa ‘Shari’ah: kwa mara ya

kwanza baada ya sulhu ya Imam Hasan (a.s.) karne 14 zilizopita, yaliwekwa na jamii

hii ambayo inamwamini kwa nguvu zote Imam al-Mahdi (a.s.).

Unadhani (mapinduzi hayo) yalikuwa ni kazi ya walio kata tamaa?

Yanaweza kuonekana kama ni kitu kigeni, lakini ndiko kutimizwa kwenyewe kwa

utabiri uliowafanya wengi miongoni mwa waislamu kukanusha kuwepo kwa al-

Mahdi katika zama hizi. Angalia, hakuna anayepingana na Wahindu, Wayahudi na

Wakristo kuhusu Avatar wao wa 10 au Masiya. Ni kwa sababu wote hao si jambo la

uhakika la wakati huu, wao kwa sasa si chochote isipokuwa ni dhana (fikra),ambayo

haiwezi kuwadhuru (watu) waovu. Lakini al-Mahdi si dhana; yeye ni (kitu) halisi

(kilichopo), ni uhakika (ambao upo),ni mtawala aliye hai, aliye tayari wakati wote

kuja kuhukumu baina ya dhalimu na mwenye kudhulumiwa,na hali hiyo

inawasumbua watu wengi wasiokuwa tayari kujisalimisha (wenyewe) mbele ya

utawala wa Allah. Wao kama alivyo yule mbuni anayepigiwa mfano - wanajaribu

kujiokoa kwa kuufumbia macho ukweli halisi na kupinga hali halisi ilivyo.

Sasa ni wazi kwamba, kumuamini al-Mahdi na kuamini kuwa atauweka utawala wa

Mungu ardhini kunategemea msingi imara wa hadithi za Mtume (s.a.w.w.)

zilizopokelewa mwanzoni kabisa mwa Uislamu na Muhaddithun wa Kisunni na

Kishia: na kwamba sio ndoto za mchana za wanachuoni wa Kishia, ambaowana

daiwa kuchuwa hifadhi katika imani hiyo kwa sababu kudhihiri kulikotarajiwa kwa

Imam wa 12 hakukutokea haraka.

Sasa, inapendekezwa kuonyesha kwamba ghaybah (kutoonekana) ya Imam al-Mahdi

(a.s.) haikuwa ni jambo lisilotarajiwa; lilitabiriwa na ‘Ali (a.s.) na Maimamu wengine

wa Ahlul-bayt, vitabu viliandikwa na mashairi yalitungwa mahsusi kwa ajili ya jambo

hili muda mrefu kabla ya kuzaliwa kwa Imam al-Mahdi (a.s.).

Hebu tuanze na Qasidah ya mshairi mashuhuri wa Ahlul-Bayt, As-Sayyid Ibn

Muhammad al-Himyari, iliyotungwa miaka mia moja na hamsini kabla ya “ghayba”,

katika zama za Imam Ja’far as-Sadiq (a.s.)

Kwanza (hebu tutoe) maelezo machache kuhusu as-Sayyid:

Abu Hashim Isma’il Ibn Muhammad al-Himyari (maarufu kama as-Sayyid) alizaliwa

mwaka wa 105 A.H., Oman, kwa wazazi wa kiibadhi, lakini aligeuka kuwa Mshia

utotoni mwake na akabaki imara (na madhubuti) katika imani yake, pamoja na

shinikizo na dhulma ya wazazi wake ambayo ilimlazimisha kuhama nyumba yake ya

mjini Basrah.

Alikwenda kuishi mjini Kufa ambako alipokea haithi kutoka kwa Al-A’mash na

wengineo. Aliishi katika zama za makhalifa 10, (watano katika Bani Umayyah, na

watano katika Bani Abbas); na alifariki Baghdad katika utawala wa Harun ar-Rashid

mwaka 173 A.H. (au 178 au 179).

Yeye ni miongoni mwa “washairi wakubwa” watatu katika Uislam. Inaeezwa hapo

mwanzo kwamba, ushairi ulikuwa ni kitu kilichokuwa karibu sana na mioyo ya

Waarabu (wanachokipenda sana) na shairi zuri au Qasidah likizagaa (na kuenea)

haraka sana kama moto wa kiangazi miongoni mwa Waarabu kwa muda mfupi sana

(wa kustaajabisha). Pia ilikua ni rahisi kulikumbuka na kusimulia.

Jina la as-Sayyid, na umashuhuri wake ulikuwa umeenea ndani ya Ulimwengu wa

Kiislamu; na uwezo mkubwa wa kujieleza aliokuwanao ulikuwa hauna mfano katika

historia. Watu wengi walifanya kuwa jukumu lao kuhifadhi na kusoma mashairi

yake. Watu kama hao walikuwa wakiitwa Rawiyah, na kila mshairi maarufu alikuwa

na Rawiyah wake, lakini as-Sayyid alikuwa na Rawiyah kumi na wawili. 4

Hapo mwanzo as-Sayyid alikuwa akifuata Imani ya Kaysariyyah ya kwamba

Muhammad Ibn al-Hanafiyyah alikuwa ni Imam wa nne na kwamba aliingia ndani ya

ghaybah (kutoonekana) na atadhihiri tena karibuni na Qiyamah. Baadhi ya mashairi

yake katika mada hii yamehifadhiwa ndani ya vitabu. Kisha alikutana na Imam Ja’far

as-Sadiq (a.s.); na baada ya kuziona dalili zilizowazi kutoka kwa Imam Ja’far as-

Sadiq (a.s.), aliifuata njia iliyonyooka na akaiacha Imani ya Kaysariyyah.

Kwa kuikubali Imani ya haki, alisoma Qasidah mbalimbali ndefu mashuhuri kuhusu

suala hilo. Ya kwanza inaanza na mistari hii:-

“Nilipowaona watu wanapotea katika dini, nilimfuata (Imam) Ja’far (as-Sadiq)

pamoja na wale wanaomfuata.”

Na nililiita (na kulitaja) jina la Allah, na Allah Mkuu-. Na ninaamini kwa dhati kuwa

anasamehe na kuhurumia. 5

Kisha alitunga (Qasidah) nyingine, akielekeza kwa Imam (a.s.) ambayo ndani yake

anaelezea ni kwa nini alipotezwa (na kuingia) ndani ya imani ya Kaysariyyah:

Anasema:-

4 Kwa maelezo zaidi ju ya maisha ya as-Sayyid, angalia vitabu vya fasihi vya historia ya Arabia.

Taarifa muhimu - pamoja na rejea kamili inaweza kupatikana ndani ya “al-Ghadir” (cha marhum”

Allamah al-Amini). J. 2 uk. 213 - 289; chapa ya 3. Angalia pia:-

(a) Al-Kashshi, “Ikhtiyarn Rijali’l-kashshi” ( Mu’assasah ‘Ahlil-Bayt li Ihya’it turath. Qum), 1404

A.H., J. 2 uk. 569 - 574.

(c) As-shaykh at-Tusi, “al-Fihrist,” (kilichochapishwa tena, kwa off-set,toleo la Najaf),

hakina tarehe, uk. 82.

5 al-Amini, al-Ghadir, uk.244-246.

Ee Wasii wa Allah na mtoto wa Wasii wake! Natubu kwa Mungu Mwingi wa rehema,

na kisha narejea kwako baada ya jambo lile ambalo nililiamini kwa nguvu (zangu

zote) na ambalo nilikuwa nikilipigania (yaani nikajadiliana) na kila mtu.

Na nilipokuwa na Imani kumhusu mtoto wa Khawlah (Muhammad al-Hanafiyyah)

kwamba alikwa amejificha, haikuwa ni kwa sababu (Mungu apishe mbali) nilikuwa

na uadui kwa kizazi cha aliyetakaswa (yaani kwa Imam Zaynul’Abidin (a.s.))

Lakini (ni kwa sababu) tuliletewa habari kutoka kwa Wasii wa Muhammad

(yaani kutoka kwa Ali a.s.) na hakuwa ni muongo kwa yale ayasemayo; “Waliyul

Amri” (Bwana wa mambo yote) atapotea - hataonekana- (akibakia) ndani ya

maficho, kama afanyavyo mtu ambaye ni muangalifu na mwenye kungojea;

Na milki ya aliyepotea itagawanywa (baina ya jamaa zake) kana kwamba

amezikwa sehemu iliyoinuliwa (yaani kaburi);

Kwa atakuwa hivyo kwa muda, kisha atainuka ghafla kama nyota, Thuraya,

inavyochomoza angani.

Ataelekea kwa msaada wa Allah kutoka katika Nyumba ya Mola wake, kwa

utukufu wa Kimungu na mamlaka yaliyopangwa vema;

Atasonga mbele (akiwa) na bendera yake kuelekea kwa maadui zake, na

atapambana nao kwa upanga na kuwamaliza (wote), kama afanyavyo mtu mwenye

nguvu aliyekasirishwa.

Ee, tulipoambiwa kuwa mwana wa Khawlah (Muhammad al-Hanadiyyah)

amejificha, tulitumia neno letu (yaani hadithi hiyo hapo juu) kwake, na

hakulikanusha).

Na tulisema kuwa yeye ni Mahdi na ni Qa’im,ambaye kwa uadilifu wake kila

mtu masikini (mwenye njaa) ataishi (kwa raha).

Lakini ukisema, “Hapana,” kwahiyo ukweli ni (kile kitu) unachokisema; na

ulichokiamrisha ni haki - bila shaka (yoyote). Na namfanya Mola wangu (kuwa) ni

Shahidi kwamba neno lako ni hoja (yaani mamlaka) juu ya kila kiumbe, wawe ni

watii au waasi.

Kwamba Bwana wa mambo yote, na Qa’im (ambaye kwake moyo wangu

unatamani kwa shangwe).

Atapata ghaybah, ni muhimu (kwake) kutoweka na kuingia kwenye ghaybah hiyo -

Allah amshushiie rehema zake, (mtu huyo) aliyejificha.

Kisha atakuwa (akingojea kama hivyo); kisha atadhihiri katika zama zake na

ataijaza mashariki na magharibi kwa uadilifu.

Hivi ndivyo (ninavyoamini sasa) kwa siri na dhahiri, Ee Wasii wa Allah! na

sijali ikiwa nitalaumiwa kwa hilo.6 ”

Ash-Shaykh al-Mufid anafafanua juu mistari hii. "Angalia tamko hili la as-

Sayyid ambalo linataja wazi ghaybah. Ana wezaje kulisema (katika hali ya uwazi

kama hiyo); je, hakulisikia kutoka kwa Maimamu wake (a.s.) na Maimamu wake

wamelisikia kutka kwa Mtume , rehema na amani ya Allah iwe juu yake na kizazi

chake. Vinginevyo, iliwezekanaje kwa mzungumzaji kuelezea kitu fulani na kisha

6 al-Amini, al-Ghadir, uk. 400-401

(kwa) kitu kicho kutokea vile vile kama alivyosema. Bila ya kukosea hata herufi

moja?.”7

Katika usuli huu, na kwa kuzingatia kuchomwa (kuunguzwa) maktaba za kishia mara

kwa mara kuanzia karne ya nne ya hijirah (viliochomwa vitabu vya maktaba isiyo

mfano ya Sheykh at-Tusi kwa mara nyingi) hadi sasa (pindi majeshi ya Israeli

yanayoikalia kusini ya Lebanon yalipoiunguza maktaba ya marhum as-Sayyid

Muslim al-Amin al-Amil, iliyokuwa na maelfu ya miswada - maandishi ya mkono -

adimu yasiyopatikana kwengineko), beti hizo zilizo tajwa hapo juu za as-Sayyid, hata

kama hazikubaliwi na hoja nyingine yeyote, ingetosha kuthibitisha kuwa ghaybah ya

Imam al-Mahdi ilikuwa ni tukio lililotabiriwa (hapo mwanzo) na Mtume na

Maimamu (rehema na amani iwe juu yake na juu yao) hasa kwa kuwa (beti) hizo

zilielekezwa kwa Imam Ja’far as-Sadiq (a.s.) zikisema kwamba ni Imam (a.s.) ndiye

aliyemwambia maneno hayo as-Sayyid al-Himyari. Lakini tunazo vile vile “hadithi”

za Maimamu kuhusu jambo hilo, moja wapo ikiwa imetajwa hapa kutoka ndani ya

kitabu cha ash-Shaykh al-mufid “Risalah ya tano kuhusu Ghayba” kidogo.

Ameandika:-

"Ya kwanza kati ya hizo ni hadithi iliyosimuliwa kwa pamoja na Masunni na Mashia;

na imetaarifiwa na kumayli ibn Ziyad. Anasema: “Nilimwendea (siku moja)

kiongozi wa waumini (Ali a.s.), na alikuwa anakwangua juu ya ardhi, nikamwambia:

“Ee Bwana wangu! kwa nini waikwangua ardhi? Je, ni kwa sababu ya wewe

kuipenda?” Akajibu (akasema); Naapa kwa Mungu! Sijawahi kuitamani hata siku

moja. Lakini nilikuwa nikimfikiria (mtu) wa tisa katika kizazi (wajukuu) wa Huseini

(a.s.). Ni yeye ndiye atakayeijaza ardhi kwa usawa na uadilifu, baada yakuwa imejaa

dhulma na ujeuri. Atakuwa na ghaybah (kutoonekana) ambayo ndani yake waongo

watatia shaka (ya kuwepo kwake). Ee kumayl, mtoto wa ziyad, ni muhimu kwa ardhi

kuwa na shakhsiya inayofahamika, au aliyejificha (na) asiyejulikana -ili kwamba hoja

za Mungu zisikatike.”

Al-Mufid anasema kuwa: “Hadithi hiyo ni ndefu, tumetaja hapa sehemu

inayohusu mada yetu.”8

Lazima itajwe kwamba, kama mwijibu wa Shaykh al-Mufid, hadithi hii

imesimuliwa na wapokezi wa Kisunni pia katika siku hizo za mwanzo. Asingeweza

kutoa dai hilo kiurahisi wakati anafahamu kuwa maadui wa imani yake

wangemshambulia lau angeandika walau neno moja la ushahidi,au kutoa dai lisilo na

msingi.

Hadithi (zisemazo) kuwa al-Qa’im al-Mahdi atakuwa amejificha mbali na

watu kwa muda mrefu sana. Jambo ambalo litawafanya watu wengi wapotee -

(hadithi hizo) zilikuwa zikizunguuka katika ulimwengu wa Kishia tokea siku za Imam

Ali (a.s.).

7 al-Mufid Risala ya tano juu ya Ghaibah, uk. 400-401.

8 al-Mufid, Risala ya tano juu ya ghaibat, uk 400.

Mbali na maneno yaliyokuwa wazi, yaliyofafanuliwa na yasio na utata

wowote ya as-Sayyid al-Himyari, kuna matukio mengi ya kihistoria ambayo

yanathibitisha mara nyingine tena kuwepo kwa hadithi hizo na athari zake.

Wakati Imam Musa al-Kadhim (a.s.) alipofariki katika mwaka wa 103/1799, baada ya

kupitisha muda mrefu katika gereza la Harun an-Rashid, kiasi kikubwa cha pesa zake

(Imam) kilikuwa kimelimbikizwa na mawakala wake wengi waliokuwa katika miji

mbali mbali. Miongoni mwao Ziyad Qandi alikuwa na dinari elfu moja , na ‘Ali Ibn

Abi Hamzah al-Bata’ini alikuwa na elfu thelathini. Wao na wengine wengi mfano

wao walizitumia pesa hizo kimakosa (kiharamu) katika kuwekeza kwao na katika

matumizi ya nyumbani.

Wakati Imam ar-Ridha (a.s.) alipowaandikia mawakala hao akiwaamuru kuzirudisha

pesa hizo kwake, wengi wao walihisi kunaswa. Na njia rahisi zaidi waliyoiona wao

ya kujikwamua ilikuwa ni kukanusha kifo cha Imam Musa al-Kadhim (a.s.).

Wakasema kuwa Imam al-Kadhim (a.s.) alikuwa ni al-Qa’im al-Mahdi, ambaye

amejificha. kama zinavyoelezea ahadithi za Maimamu waliotangulia wakisema kuwa

la-Mahdi atabaki (hali ya kuwa) amejificha; wakadai kwamba ni Imam al-Kadhim

(a.s.) ndiye aliyekuwa al-Mahdi na sasa alikuwa ndani ya ghaybah. Huu ndio

uliokuwa mwanzo wa madhehebu ya Waqifah.9 Tunachohusika nacho hapa, ni ukweli

wa kwamba baadhi ya viongozi wa kundi la Waqifah waliandika vitabu kuhusu

ghaybah; ambavyo ndani yake wameziorodhesha hadithi zilizopokelewa kutoka kwa

Maimamu kuhusu ghaybah, twabaan, walijaribu kimakosa kuzihusisha kauli hizo na

Imam Musa al-Kadhim (a.s.) (yaani kwamba zamhusu yeye). Mmoja wao alikuwa al-

Hasan Ibn Muhammad Ibn Sama’ah ul-kufi, aliandika vitabu thelathini, kimoja wapo

kikiwa “kitabu al-Ghaybah. Alifariki mwaka 263 A.H., miaka mitatu baada ya kifo

cha Imam wetu wa 11 Hassan al-’Askari (a.s.). “Kitabu al-ghaybah” chake

kilikuwepo katika vituo (maeneo) vya kishia, as-Shaykh at-Tusi (ambaye alikuwa na

Ijazah ya kauli hadithi) alikuwa na nakala (yake) katika maktaba yake, kama

inavyoweza kuonekana katika “al-Fihrist” (Faharasi) yake. 10

Hadithi hizi zilikuwa zinafahamika sana kiasi ambacho waandishi wengi wasokuwa

Mashia walizikusanya katika muundo wa kitabu. Nimekitaja kitabu kimoja hapo

mwanzo, vitabu vingine vitatu vinatolewa apa:-

1. ‘Ubbad Ibn Ya’qub ar-Rawajini alikuwa ni “muhaddith wa Kisunni aliyefariki

mwaka wa 250 A.H. yaani wakati wa uhai wa Imam wa 10, ‘Ali an-Naqi (a.s.).

Aliandika kitabu “Kitab Akhbat al-Mahdi” (kitabu cha hadithi kumhusu al-Mahdi

a.s.).11

9 . Al-Kash-sh, (op.cit.) uk. 755 - 774; 705 - 707; 742 - 744; an- Nijashi, “al-Fihrist”, Qum 1398, uk.

Al-Khoui, “Mujam Rijal al-hadithi”, Najaf, 1975, J.m. uk. 229 - 246.

10 at-Tusi, uk. 51-52

11 Ibid; uk. 119-120

2. Muhammad Ibn al-Hasan Ibn Jamhur al-’Ammi al-Basri alikuwa ni sahaba wa

Imam wa 8 ‘Ali ar-Ridha (a.s.) aliyepokea baadhi ya hadithi kutoka kwake.

Alikuwa ni”Ghaliy”.12 Aliandika vitabu vingi. Viwili miongoni mwa vitabu

vyake vinaitwa: (a) “Kitab Sahib iz-Zaman a.s.; na (b) Kitab Waqf Khuruj al-

Qa’im a.s. (yaani kitabu cha wakati wa kudhihiri kwa al-Qa’im a.s.) .13

3. Mashi’a walikuwa mara nyingi wakiwauliza Maimamu (a.s.) kuhusu viongozi

wa madhehebu za Waqifah na nyinginezo mfano wake, ni nini yawapasa

wafanye kuhusu vitabu vyao. Jibu lilikuwa wakati wote ni lile lile (chukueni

hadithi zao, na acheni kando maoni yao). Ni kwa sababu hiyo ndiyo ma ‘ulama’

wetu walikuwa wakizichukua hadithi zilizopokelewa na wasio Mashia

Ithna'shariyyah pia (ilimradi zimetimiza masharti mengine muhimu). Na

ninafurahi kwa wao kufanya hivyo, na wala si kwa sababu tu ya kumbukumbu za

kihistoria.

4. Kwa kusimulia “Kitab ul-Ghaybah” cha al-Hasan ibn Muhammad Ibn

Suma’ah na vile vitabu vya (watu wengine na kuwaingiza ndani ya “al-Fihrist”

yake, ash-Shaykh at-Tusi, alivifunga vinywa vya wale wanaodhani kuwa

kwanini Ghaybah ya al-Mahdi al-Qa’im ilikuwa ni njama ya Maulamaa wa

Kishia iliyopangwa pindi kudhihiri kulikokuwa kukitarajiwa kwa Imam wa 12

(a.s.) hakukujitokeza. Vitabu hivi visivyokuwa vya Kishia vyatosha

kuthibitisha kuwa kuamini kwamba al-Qa’im al-Mahdi (a.s.) atabaki ndani ya

Ghaybah (kificho) kulikuwa na turathi ya pamoja kwa Waislam wote -

Masunni na madhehebu nyingine za Kishia; na kwamba vitabu viliandikwa juu

ya maudhui hii muda mrefu kabla ya (hata) kuzaliwa Imam wa 12 (a.s.).

maoni

Acha Maoni

*Mashamba alama ya asteriski ni hakika kuwa thamani.