UTAFITI WA WANAZUONI WAKIMAGHARIBI

UTAFITI WA WANAZUONI WAKIMAGHARIBI

Makala zinazohusiana

UTAFITI WA WANAZUONI WAKIMAGHARIBI JUU YA IMAM MAHDI(a.s)

UTAFITI WA WANAZUONI WAKIMAGHARIBI JUU YA IMAM MAHDI (A.S)
Ni miaka mingi sasa wanazuoni wakimagharibi wako mbioni katika kuupekua Uislamu na kutaka kujua siri zilizomo ndani yake, wamejaribu sana kutaka kujua siri ya Qurani, Mtume (s.a.w), utmaduni wa kiislamu, Maimamu, pamoja na matokeo mengine ya kitarehe yaliomo ndani ya tarehe ya kiislamu.Walifanya hivyo huku wengi wao wakiwa ni wenye kushangazwa kutokana na walioyasikia, na wengine wakitaka kutafuta aibu fulani ili wapate sababu y kuupaka matope Uislamu, na miongoni mwa watafiti hawa wamo wale waliopendezwa na Uislamu na mwishowe wakaamua kutafsiri (kutarajumu) baadhi ya vitabu vya dua, kama vile Sahifatu-Sajjaadiyya pamoja na Dua ya Arafa.
Katika karne ya kumi na nane utafiti kuhusiana na Uislamu ulielekea katika mada inayohusiana na Mkombozi atakayekuja katika mwishoni mwa dunia, na kwa bahati nzuri suala hili la kuja kwa Mkombozi, ni moja kati ya masuala yanayozihusisha dini zote, kwani dini zote zinaamini kua kuna Mkombozi atakayekuja mwisho wa dunia.
Na miongoni mwa Wamagharibi waliofanya juu ya suala hili wamelezea kua, itikadi juu ya kuwepo kwa Mkombozi (Imam Mahdi) hasahasa ipo kwenye Dhehebu la Kishia. Lakini ukweli ulivyo ni kua itikadi haitokani na Mashia peke yao, bali madhehebu mengine vile vile yana itikadi kama hiyo.
DAVID SAMUEL MARGOLIOUTH naye ni mmoja

maoni

Acha Maoni

*Mashamba alama ya asteriski ni hakika kuwa thamani.