Sheikh Saffar akijibu dharau ya khatibu wa Msikiti wa Madina.

Sheikh Saffar akijibu dharau ya khatibu wa Msikiti wa Madina.
Maulamaa wa Kiwahabi wanataka kuzusha fitina za kimadhehebu.

 

Rpoti ya ABNA Kiongozi wa Waislamu wa madhehebu ya Shia nchini Saudi Arabia Sheikh Hassan Saffar amejibu dharau ya khatibu wa Masjidunnabi SAW kwa Waislamu wa madhehebu ya Shia nchini humo akisema kuwa maulamaa wa Kiwahabi wanataka kuzusha fitina za kimadhehebu.

Khatibu wa Msikiti Mtukufu wa Madina Sheikh Ali Hudhaifi jana aliwashambulia na kuwavunjia heshima Waislamu wa madhehebu ya Shia katika hotuba za Swala ya Ijumaa, jambo ambalo limekosolewa na Sheikh Hassan Saffar, imamu wa Swala ya Ijumaa ya mji wa Qatif huko mashariki mwa Saudi Arabia. Sheikh Saffar amesema mahatibu wa Kiwahabi wana nia ya kuzusha fitina za kimadhehebu na mapigano ya kimakundi.

Kiongozi wa Mashia wa Saudi Arabia amesema baadhi ya watu wanatumia vibaya maandamano yanayofanyika katika mji wa Awamiya huko mashariki mwa Saudi Arabia kwa malengo ya kimadhehebu na kuwashambulia wafuasi wa madhehebu ya Shia. Amesisitiza kuwa suala hilo halina maslahi ya Saudia.

Sheikh Hassan Saffar amemuuliza Sheikh Ali Hudhaifi na mahatibu wengine wa Kiwahabi kwamba, kwa nini Waislamu wa madhehebu ya Shia wanazuiwa kusimamisha Swala za jamaa katika miji na maeneo wanakoishi? Kwa nini Mashia wanapodhalilishwa na kuvunjiwa heshima ndani ya Masjidul Haram hakuna mtu anayelaani vitendo hivyo viovu? Kwa nini Shia anapofariki dunia haruhusiwi kuzikwa mahala wanapoishi? Kwa nini Mashia hawapewi nafasi za kazi katika idara za serikali ya Saudi Arabia? Na kwa nini Mashia hawaruhusiwi kuingiza maiti zao ndani ya Msikiti wa Mtume mjini Madina?

Sheikh Saffar amesema, hadi sasa hatujasahau kwamba serikali ya Saudia ilizuia kuingizwa maiti ya kiongozi wa Mashia wa Madina Ayatullah Sheikh al Amri katika Msikiti wa Mtume.

maoni

Acha Maoni

*Mashamba alama ya asteriski ni hakika kuwa thamani.