Fitina za Mawahabi katika mji mtakatifu wa Karbala

Fitina za Mawahabi katika mji mtakatifu wa Karbala
olisi ya Iraq imetangaza kuwa silisila ya milipuko ya mabomu imeutikisa mji huo mtakatifu hususan karibu ya jengo la serikali za mitaa linaloshughulikia masuala ya vitambulisho na hai za kusafiria.

 

Rpoti ya Shirika la Habari la Ahlul Bayt(a.s)-ABNA Ikieleza kuwa; Polisi ya Iraq imetangaza kuwa silisila ya milipuko ya mabomu imeutikisa mji huo mtakatifu hususan karibu ya jengo la serikali za mitaa linaloshughulikia masuala ya vitambulisho na hai za kusafiria.

Mashambulizi hayo ya kigaidi yamesababisha vifo vya watu wasiopungua 12 hadi sasa na kujeruhi wengine zaidi ya 100.

Afisa mmoja wa polisi ya Karbala amesema kuwa mlipuko wa kwanza ulitokea asubuhi saa tatu na nusu, na wakati watu walipokuwa wakiwasaidia majeruhi, magaidi walilipua milipuko mingine mitatu.

Baada ya milipuko hiyo ya kigaidi, polisi ya Karbala imefunga njia zote za kuingia na kutoka katika mji huo mtakatifu ili kuzuia mashambulizi zaidi kama hayo.

Viongozi wa Iraq wamekuwa wakiilaumu Saudi Arabia kwamba inafadhili makundi ya Kiwahabi yenye misimamo mikali inayotekeleza mashambulzi ya kigaidi katika maeneo matakatifu ya Kiislamu nchini Iraq.

maoni

Acha Maoni

*Mashamba alama ya asteriski ni hakika kuwa thamani.