MTUME KATIKA NDIMI ZA WAMAGHARIBI

MTUME KATIKA NDIMI ZA WAMAGHARIBI

Makala zinazohusiana

Washington Irving (1783-1859 )Anayejulikana kama "The first American man of letters": " "Alikuwa na tabia tulivu na mwenye nidhamu katika chakula, na akifuata sana utratibu wa kufunga. Hakuvama katika kupenda mavazi ya mapambo, namna wanavyojionyesha wenye mawazo finyu; pia kunyenyekea kwake katika mavazi kuliathiri pia kulionyesha matokeo ya kutopenda kwake kujitofautisha... alikuwa muadilifu katika muamala wake wa kibinafsi. Aliamiliana na watu wote kwa usawa: marafiki na wageni, matajiri na maskini, na wenye nguvu na wanyonge; na alipendwa na watu walala hoi kwa kuwa jinsi alivyokuwa akiwapokea kwa vizuri, na kusikiliza matatizo yao... Ushindi wake wa kijeshi vitani haukumfanya awe na ujuba au kibri, kama ambavyo wengine wangefanya hivyo kwa kuathiriwa na ubinafsi. Alipokuwa katika enzi za utawala wake wenye nguvu, aliendelea kujiweka kinyenyekevu kama alivyokuwa katika siku za shida. Alijiweka mbali na heshima kuu ya uongozi na hakuwa akifurahishwa iwapo ataingia mahali na apewe heshima kuu mno."
[Life of Mahomet, London, 1889, Uk. 192-3, 199]Annie Besant (1847-1933) Mwingereza na kiongozi India.Pia Rais wa chama cha Indian National Congress mnamo mwaka 1917: " "Haiwezekani kwa atakayesoma maisha na tabia za Mtume mkuu wa Arabia, akajua vipi alifundisha na vipi aliishi, kuhisi chochote ila atahisi utukufu aliokuwa nao mtume huyo mkuu, mmoja kati ya wajumbe wakuu wa Mungu. Japo nitakayokueleza yatakuwa ni mengi yaliyozoeleka kwa watu wengi, lakini mimi binafsi ninapoyarudia kuyasoma nahisi kuyapenda upya na napata kuhisi heshima kubwa juu ya mwalimu huyo mkuu wa Arabia." [The Life And Teachings Of Muhammad, Madras, 1932, Uk. 4]


Edward Gibbon (1737-1794) Anayechukuliwa kuwa ndiye mwanahistoria mkuu wa enzi zake. " "Alikuwa (Muhammad) na kumbukumbu pana na nzuri, mzaha wake ulikuwa wa kawaida na wa kushirikiana na watu, mwenye mawazo yenye kutia moyo, maamuzi yake yalikuwa ya wazi, ya haraka na ya kukata. Alikuwa na ujasiri wa kufikiri na kutenda." [History of the Decline and Fall of the Roman Empire, London, 1838, Juz. 5, Uk. 335]
Muhammad si baba wa yeyote katika wanaume wenu, bali yeye ni Mtume wa Mwenyezi Mungu na Mwisho wa Mitume (Qur'an 33:40) Wasio Waislamu wanasema nini juu ya

maoni

Acha Maoni

*Mashamba alama ya asteriski ni hakika kuwa thamani.