Ukafiri wa Mawahabi

Ukafiri wa Mawahabi

Je! kunauhusiano gani wa Aya ya 36 ya Surat Yusuf na Kutiwa Jela Husni Mubarak?

Ripoti ya Shirka la Habari la AHlul bayt(a.s)-ABNA- Aidh al Qarani ambaye ni miongoni mwa mamufti wakubwa wa Kiwahabi wa Saudi Arabia ametoa mtazamo wa kuchekesha kwa kufananisha kuingia dikteta wa Misri Hosni Mubarak na wanawe wawili mahakamani na jinsi Nabii Yusuf AS na vijana wawili walivyoingizwa jela!

Kituo cha habari cha Nasij kimeripoti kuwa, Sheikh Aidh al Qarani ambaye alikuwa akifasiri aya ya 36 ya suratu Yusuf amesema, jinsi ya kuingia mahakamani Hosni Mubarak na wanawe wawili Alaa na Jamal, ni sawa kabisa na alivyoingia jela Nabii Yusuf AS na vijana wawili!

Akifasiri aya hiyo inayosema: «وَدَخَلَ مَعَهُ السِّجْنَ فَتَیَانَ» "Na waliingia jela pamoja naye vijana wawili", shekhe huyo wa Kiwahabi wa Saudi Arabia amemshabihisha dikteta aliyeng'olewa madarakani nchini Misri Hosni Mubarak na Nabii Yusuf AS, na watoto wake wawili wamefananishwa na vijana waliokuwa pamoja na Nabii huyo wa Mwenyezi Mungu.

Aya hii inaashiria vijana wawili ambao mmoja alihusika na chakula cha mfalme wa Misri na mwingine alishughulikia vinywaji vyake, na shekhe huyu wa Kiwahabi ametabikisha aya hii kwa Alaa na Jamal, wana wa Mubarak na kuwafananisha na watu waliokuwa wakidhamini chakula cha taifa la Misri.

Tafsiri na matamshi hayo ya mufti wa Kiwahabi yamewakasiri mno hata baadhi ya maulamaa wa Saudi Arabia kama Ahmad al Arfaj ambaye amemtuhumu Sheikh al Qarani kwamba anafasiri aya za Qur'ani Tukufu kwa mujibu wa matakwa yake binafsi.

maoni

Acha Maoni

*Mashamba alama ya asteriski ni hakika kuwa thamani.