Sisi na Masuni tupo udande mmoja na Mawahabi wapo upande wao

Sisi na Masuni tupo udande mmoja na Mawahabi wapo upande wao

Kikao cha Tatu cha kukurubisha chenye Anuani ya “Njia sahihi za mahusiano za Mashia na Masuni” Kikao hicho kikihudhuriwa naAyatullah Allamah Sayyid Kamal Haidariy.

Ripoti ya Shirika la Habari la Ahlul Bayt(a.s)-ABNA- Sayyid Kamal Haidariy alisema:kwanini tujishughulishe na uhusiano wa Mashia na Masuni Badala ya kuzungumzia Masuala ya Muhimu! Mashia sasa tuna masuala ya Muhimu ya kuzungumzia kwani tunamatatizo mengi ya Kiitikadi, tutawezaje kuzungumzia katika masuala ya Uhusiano na wengine?! akiendelea kusema kuwa suala la Uhusiano ni suala pana sielewi nianze na lepi kwani sasa hata bado hakujafahamika Maana Masuni ni nini?!.

 

Katika Dunia wapo zaidi ya Milioni 400 ya Masuni na baina yao kuna Fikra nyingi za kiitikadi.

 

Ayatullah Haidariy: katika Ukumbi wa Imam Musa Sadr katika Chuo kikuu cha Dini na Madhehebu akisema Ibn Taimia ni Mtu alieweka athari Mbaya katika Ulimwengu, katika Miaka 100 ya hapa karibuni zaidi ya makala 240 kunako Ibn Taimia, pia kuandika Mshia mmoja Vitabu 24 kuhusu Shakhsia hii.

 

Sayyid Kamal Haidariy alizidi kuwekea mkazo kuwa Ulimwengu wa sasa ni Ulimwengu ulioendelea Ulimwengu wa Mawasiliano na kikiandikwa Kitabu au Matlabu hayawezi kufichika na kutofahamu Watu. Tunamshukuru Mwenyezi Mungu kwa maendeleo haya ya Hauza.

 

Pia alizungumzia kunako Uwahabi kuwa umeathirika na Fikra za Ibn Taimia na kuja Mtu aitwae Muhammad Ibn Abdulwahab kuzagaza Fikra za Ibn Taimia ila Fikra za Muhammad Ibn Abdulwahab hazikuwa moja kwa moja za Ibn Taimia kwani Muhammad Ibn Abdulwahab alikuwa ni mfataji na mfasi tu asiejua chochote kile kunako Fikra za Ibn Taimia lakini yeye alikuwa ni mwana siasa tu aliekuja kuvamia Fikra za Ibn Taimia.

 

Allamah Haidariy kuathiri fikra za Muawiya katika Uwahabi alisema;Makala 30 za Vyuo vikuu zinazomzungumzia Muawiya na Baadhi ya Vyuo viliandika Makala 1000, Makala zote hizi zilitumiwa na Mawahabi kutumia katika itikadi potovu zao, Banii Umaiya waliathiri sana katika kuharibu Uislamu katika Tafsiri, Fiqhi na Akida.ni lazima kuhakiki katika suala hili ila la kuhuzunisha ni kwamba katika nyanja hii bado hakuja fanyika Uhakiki.

 

Ayatullah Haidariy: Sasa Mawahabi wanadai kuwa wao ndio Mawakili wa Masuni Duniani, na kuleta Fitina baina ya Mashia na Masuni na hali ya kuwa Maktab ya Ahlul Bait(a.s) yaani Mashia wanamatatizo na Banii Umaiya na si Masuni, Mashia na Masuni hakuna tofauti, tofauti ipo kwa Banii Umaiya na Mashia.

 

Kumalizia Sayyid Kamal Haidariy alisema:Suala muhimu ni kwamba tofauti ya kiitikadi na Kifikra baina yetu si na Masuni bali ni Mawahabi, akiendelea kusema kuwa ni lazima kutenganisha baina ya Masuni na Mawahabi tija ya hii Fikra ni kwamba Sisi na Masuni tupo upande wetu na Mawahabi kuwa upande wao tutaona niwepi watakao kuwa wengi na wepi watakuwa wachache kutokana Fitina zao za Uwingi na Uchache.

maoni

Acha Maoni

*Mashamba alama ya asteriski ni hakika kuwa thamani.