HAKUNA FUNGAMANO KATIKA HILA

HAKUNA FUNGAMANO KATIKA HILA

 BISMILAHI RAHMANI RAHIYMI

KWA JINA LA MWENYEEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU

HAKUNA FUNGAMANO KATIKA HILA

3. KUTOKUWEPO FUNGAMANO LA HILA ZOZOTE.

Duniani kuna baadhi ya watu waovu, na Serikali mbovu ambazo zinaendeshwa katika mfumo usiokuwa sahihi, yaani zinaendeshwa kwa mfumo wa kishetani, serikali ambazo huongozwa kwa kuwafanyia watu dhulma, au huongozwa kwa hila ambazo huwapatia watu hao waovu ridhaa za nafsi zao, na kuwapotoa watu kifikra, watu hao huifunga njia ya Mwenyeezi Mungu, na kuwazuia waumini ili wasifanye yale ambayo Mitume imewaamrisha watu kuyafanya, ili waweze kufikia katika malengo yao mapotofu na manufaa yao wanayoyakusudia, au kufikia katika vyeo wanavyovihitajia, au kuwa na nafasi fulani katika jamii, ama siku ya Kiama ni siku ya kufichuka kila yaliyofichwa na haki kudhihirika, hakuna mtu yoyote yule atakayeweza kufanya jambo kutokana na hila zake, na hatokuwa na njia yoyote ile itakayomfanya akimbie hukumu yake atakayohukumiwa kutokana na hila zake alizozifanya ulimwenguni, basi Mwenyeezi Mungu (s.w) atawahukumu waovu hao kwa uadilifu. kama tunavyoshuhudia ndani ya Qur-ani:-

يَوْمَ لاَ يُغْنِى عَنْهُمْ كَيْدُهُمْ شَيْئاً وَلاَ هُمْ يُنصَرُونَ[1]

Siku ambayo hila zao hazitawafaa hata kidogo, wala wao hawatanusuriwa.

4. KUTOKUWEPO FUNGAMANO LOLOTE LA ELIMU POTOFU NA AKIDA BATILI.

Duniani kuna baadhi ya watu ambao ni wasomi, lakini elimu yao huitumia katika njia potofu za shirki na kufuru, watu hao huitumia elimu waliyonayo kwa ajili ya kuwaharifu watu ili wasiitambue haki na kuwaweka mbali na Mwenyeezi Mungu, baadhi ya wakati huibadilisha haki na kuiweka batili, lakini siku ya Kiama, siku ambayo ni siku ya kudhihirika kila yaliyofichwa na kudhihiri ile haki aliyoibainisha Yeye Mola Mtukufu, na kubatilika yale yote yaliyobainishwa kwa upotofu, na wale wasomi waliyoitumia elimu yao kwa ajili ya kupigania akida zao batili, na kuwazulia Mwenyeezi Mungu na Mitume yake uwongo, basi  siku hiyo (Kiama) kanuni na sheria ni zake Mola Mtakatifu tu, na elimu zote potofu zitateketezwa kwa uwezo wake Allah (s.w). katika Qur-ani tunasoma:-

وَنَزَعْنَا مِن كُلِّ اُمَّةٍ شَهِيداً فَقُلْنَا هَاتُوا بُرْهَانَكُمْ فَعَلِمُوا اَنَّ الْحَقَّ لِلَّهِ وَضَلَّ عَنْهُم مَّا كَانُوا يَفْتَرُونَ[2]

Na tutatoa shahidi katika kila umma, na tutasema: Leteni hoja zenu! Hapo watajua kwamba hakika kweli ni ya Mwenyezi Mungu, na yatawapotea yale waliyo kuwa wakiyazua.

 

[1] Surat Tuur Aya ya 46.

[2] Surat Al-Qasa Aya ya 75.

maoni

Acha Maoni

*Mashamba alama ya asteriski ni hakika kuwa thamani.