IMAMU ALI (A.S) KATIKA MTAZAMO WA WASIOKUA WAISLAMU

IMAMU ALI (A.S) KATIKA MTAZAMO WA WASIOKUA WAISLAMU

Simon Ockley (1678-1720) Profesa wa lugha ya kiarabu katika chuo kikuu Cambridge:
" "Jambo moja maalum ambalo lapaswa kugunduliwa kwa Ali, ni kwamba mama yake alimzaa Makka ndani ya Al-Kaaba, ambapo haijawahi kutokea kwa mtu yeyote."
[History of the Saracens, London, 1894, Uk. 331]


Washington Irving (1783-1859) Aalijulikana kama "The first American man of letters":
" "Ali alikuwa anatokana na tawi lenye heshima kuu katika matawi ya kikureishi. Alikuwa na sifa tatu zilizokuwa zikitukuzwa sana kwa waarabu: Ujasiri, ufasaha na ukarimu. Moyo wake usio na hofu ulimpatia sifa kutoka kwa Mtume ya kuwa simba wa Mungu, mifano ya ufasaha wake imebaki katika baadhi ya semi na kuhifadhiwa miongoni mwa waarabu; na ukarimu wake ulionekana dhahiri katika kupenda kwake kugawanya na watu, kila siku ya ijumaa, kile kilichobaki katika hazina. Kuhusu utukufu wake, tumetoa mifano mara kwa mara; utukufu wake ulichukia kila kitu chenye udanganyifu na uchoyo."
[Lives of the Successors of Mahomet, London, 1850, Uk. 165]


" "Yeye alikuwa ni mmoja wa miongoni mwa wa mwisho na wenye thamani miongoni mwa waislamu wa kale, ambaye alikusanya nguvu ya kidini kwa ushindi akiwa na Mtume mwenyewe, na kufuata ruwaza ya mwisho kabisa ya Mtume Muhammad. Yeye ni mtu anayetajwa kwa heshima kama khalifa wa kwanza aliye kirimu na kulinda elimu. Alikuwa ndani ya mashairi yeye mwenyewe, na nyingi miongoni mwa methali na semi zake zimehifadhiwa na kufasiriwa katika lugha mbalimbali. Pete lake ulikuwa na maandishi hili: 'Ufalme ni wa Mwenyezi Mungu'. Moja katika semi zake inaonyesha jinsi alivyokuwa hathamini vivutio vinavyopita tu vya dunia, ni (kusema kwake): 'Maisha ni kivuli tu cha mawingu - ndoto ya mwenye kulala.'"
[Lives of the Successors of Mahomet, London, 1850, Uk. 187-8]Robert Durey Osborn (1835-1889) Meja wa kikosi cha the Bengal Staff Corps:
" "Pamoja naye umepotea moyo hasa na Muislamu bora ambaye Historia ya Mohammad imehifadhi kumbukumbu hiyo." [Islam Under the Arabs, 1876, Uk. 120]
Namna hii anakubainishieni Mwenyezi Mungu Aya zake ili mpate kufahamu (Qur'an 2:242) Wasiokuwa Waislamu wanasema nini juu ya

maoni

Acha Maoni

*Mashamba alama ya asteriski ni hakika kuwa thamani.