UMUHIMU WA KUFAHAMU QUR_ANI

UMUHIMU WA KUFAHAMU QUR_ANI

BISMILAHI RAHMANI RAHIYMI

KWA JINA LA MWENYEEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU

UMUHIMU WA KUFAHAMU QUR-ANI.

UMUHIMU WA KUFAHAMU MAFUNZO NA MAANA YA AYA ZA QUR-ANI.

Qur-ani kariym ni maelezo na ujumbe ulio wazi wa Mwenyeezi Mungu kwa ajili ya watu wote. Allah (s.w) anasema:-

هَـذَا بَيَانٌ لِّلنَّاسِ وَهُدًى وَمَوْعِظَةٌ لِّلْمُتَّقِينَ[1]

Haya ni maelezo yaliyo wazi kwa watu (wote) na uongozi na mauidha kwa wamchao.

Na katika sura nyengine anasema:-

هَـذَا بَلاَغٌ لِّلنَّاسِ وَلِيُنذَرُواْ بِهِ وَلِيَعْلَمُواْ اَنَّمَا هُوَ إِلَـهٌ وَاحِدٌ وَلِيَذَّكَّرَ اُوْلُواْ الاَلْبَابِ[2]

Haya yatosha (kuwa mauidha) kwa watu, ili waonywe kwayo, na wapate kujua kuwa Yeye (Mwenyeezi Mungu) ni Mungu Mmoja tu, na ili wenye akili wakumbuke.

Vile vile anasema:-

هَذَا بَصَائِرُ لِلنَّاسِ وَهُدًى وَرَحْمَةٌ لِّقَوْمِ يُوقِنُونَ[3]

Hizi ni dalili zilizowazi kwa watu (wote); nazo ni uwongofu na rehema kwa watu wanaoyakinisha.

Na katika Suratul-Baqara anasema:-

شَهْرُ رَمَضَانَ الَّذِيَ اُنزِلَ فِيهِ الْقُرْآنُ هُدًى لِّلنَّاسِ وَبَيِّنَاتٍ مِّنَ الْهُدَي وَالْفُرْقَانِ فَمَن شَهِدَ مِنكُمُ الشَّهْرَ فَلْيَصُمْهُ وَمَن كَانَ مَرِيضاً اَوْ عَلـٰي سَفَرٍ فَعِدَّةٌ مِّنْ اَيَّامٍ اُخَرَ يُرِيدُ اللّهُ بِكُمُ الْيُسْرَ وَلاَ يُرِيدُ بِكُمُ الْعُسْرَ وَلِتُكْمِلُواْ الْعِدَّةَ وَلِتُكَبِّرُواْ اللّهَ عَلـٰي مَا هَدَاكُمْ وَلَعَلَّكُمْ تَشْكُرُونَ[4]

Mwezi wa Ramadhani ambao imeteremshwa humo Qur'ani kuwa ni uwongofu kwa watu, na hoja zilizo wazi za uwongofu na upambanuzi. Basi ataye kuwa mjini katika mwezi huu naafunge. Na mwenye kuwa mgonjwa au safarini, basi atimize hisabu katika siku nyengine. Mwenyezi Mungu anakutakieni yaliyo mepesi wala hakutakieni yaliyo mazito, na mtimize hiyo hisabu, na mumtukuze Mwenyezi Mungu kwa kuwa amekuongoeni ili mpate kushukuru.

Maelezo Kuhusiana na aya ya 185 Surat Albaqarah.

Anataka Mwenyeezi Mungu tutimize hisabu hii ya siku 30 au 29 kwa kuwa ile taathira kamili ya kufunga haitimii mpaka ichukue muda wa siku kama hizi.

Tukiendelea na mada yetu ni lazima tuelewe kuwa, njia za kufahamu maelezo au ujumbe ni kusoma na kusikia, kwa hiyo kusoma na kusikia humpelekea mtu kuyafahamu yale yaliyokusudiwa katika maelezo (matini) hayo, basi bila ya kufahamu kile anachokisoma au anachokisikia kutapelekea kutofahamu maana ya matini hiyo. Kwa hiyo ili kuelewa na kuufahamu ujumbe wa Mwenyeezi Mungu ni lazima tuzisikilize na kuzisoma Aya zake, na kusoma huko au kusikiliza kunafuatana na kufahamu kile ambacho tunakisoma au tunakisikiliza, ama kwa ujumla katika darasa za Qur-ani watu wamejitosheleza na wamezoea kuisoma Qur-ani bila ya kuifahamu au kuzingatia maana yake, na kwa sababu hiyo basi hakuna vigezo wala njia za kutosheleza zilizotayarishwa ili kuondoa tatizo hilo.

Ijapokuwa ni jambo la uwazi kabisa kuwa kuna umuhimu wa kufahamu maana ya Aya za Qur-ani, ama kutokana na dalili ya kuwa watu wameghafilika na amri hiyo iliyo wazi ni vizuri tukaelezea faida ya maudhui hayo katika sehemu hii.

1. Qiraat ni neno la kiarabu lenye maana ya kusoma, na kusoma katika kila lugha kunabainisha kuyafahamu (matini) maudhui yaliyosomwa, vile vile kusoma (maudhui) au kitabu kunaleta maana ya kujuwa na kuyafahamu maudhui hayo yaliyosomwa.

Kwa hiyo kuisoma Qur-ani ni amri ya kawaida, (yaani mtu anaposoma Qur-ani anakusudia kusoma pamoja na kufahamu maana ya kile anachokisoma), kwa hakika inaeleweka wazi kuwa kusoma bila ya kufahamu amri ya kitendo hicho cha usomaji inakuwa haijakamilika.

Na kutokana na sababu hiyo basi Allah (s.w) katika Surat- Muzammil anasema:-

إِنَّ رَبَّكَ يَعْلَمُ اَنَّكَ تَقُومُ اَدْنَي مِن ثُلُثَيِ اللَّيْلِ وَنِصْفَهُ وَثُلُثَهُ وَطَائِفَةٌ مِّنَ الَّذِينَ مَعَكَ وَاللهُ يُقَدِّرُ اللَّيْلَ وَالنَّهَارَ عَلِمَ اَن لَّن تُحْصُوهُ فَتَابَ عَلَيْكُمْ فَاقْرَؤُوا مَا تَيَسَّرَ مِنَ الْقُرْآنِ عَلِمَ اَن سَيَكُونُ مِنكُم مَّرْضَي وَآخَرُونَ يَضْرِبُونَ فِى الاَرْضِ يَبْتَغُونَ مِن فَضْلِ اللهِ وَآخَرُونَ يُقَاتِلُونَ فِى سَبِيلِ اللهِ فَاقْرَؤُوا مَا تَيَسَّرَ مِنْهُ وَاَقِيمُوا الصَّلاَةَ وَآتُوا الزَّكَاةَ وَاَقْرِضُوا اللهَ قَرْضاً حَسَناً وَمَا تُقَدِّمُوا لِاَنفُسِكُم مِّنْ خَيْرٍ تَجِدُوهُ عِندَ اللهِ هُوَ خَيْراً وَاَعْظَمَ اَجْراً وَاسْتَغْفِرُوا اللهَ إِنَّ اللهَ غَفُورٌ رَّحِيمٌ[5]

Hakika Mola wako Mlezi anajua ya kuwa hakika wewe unakesha karibu na thuluthi mbili za usiku, na nusu yake, na thuluthi yake. Na baadhi ya watu walio pamoja nawe kadhaalika. Na Mwenyezi Mungu ndiye anaye ukadiria usiku na mchana. Anajua kuwa hamwezi kuweka hisabu, basi amekusameheni. Basi someni kilicho chepesi katika Qur'ani. Anajua ya kuwa baadhi yenu watakuwa wagonjwa, na wengine wanasafiri katika ardhi wakitafuta fadhila ya Mwenyezi Mungu, na wengine wanapigana katika Njia ya Mwenyezi Mungu. Kwa hivyo someni kilicho chepesi humo, na mshike Sala, na toeni Zaka, na mkopesheni Mwenyezi Mungu mkopo mwema. Na kheri yoyote mnayo itanguliza kwa ajili ya nafsi zenu mtaikuta kwa Mwenyezi Mungu, imekuwa bora zaidi, na ina thawabu kubwa sana. Na mtakeni msamaha Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe Mwenye kurehemu.

Na Mtume Muhammad (s.a.w.w) katika hadithi yake anasema:-

اقرء القرءان واعملوا به[6]

Isomeni Qur-ani na kuyafanyia amali yale yaliyoamrishwa katika Qur-ani hiyo.

Katika ufahamu unaoonekana katika hadithi hiyo itafahamika kuwa desturi ya kuisoma Qur-ani vile vile inatoa mabainisho katika kuzifahamu maana yake aya hizo, na kama tukizingatia katika Aya za Qur-ani au hadithi tutashuhudia kuwa kumeelezewa kuzingatia na kufikiria maana ya Aya hizo. Lakini katika Aya za Qur-ani hakujatolewa dasturi yoyote inayomaanisha kufahamu maana ya Aya za Qur-ani, kwa sababu katika dasturi ya kusoma vile vile kunamaanisha dasturi ya kukifahamu kile kinachosomwa.

[1] Surat Al-Imrani Aya ya 138

[2] Surat Ibrahim Aya ya 52

[3] Syrat Al-jaathiya Aya ya 20

[4] Surat Al-baqarah Aya ya 185

[5] Surat Muzzammil aya ya 20

[6] rejea kitabu Kanzul-aamali, juzuu ya 1, ukurasa wa 511, hadithi ya 2270

MWISHO

maoni

Acha Maoni

*Mashamba alama ya asteriski ni hakika kuwa thamani.