Wapalestina: Marekani inafanya njama za kukwamisha kutambuliwa Palestina

Wapalestina: Marekani inafanya njama za kukwamisha kutambuliwa Palestina
Viongozi wa Palestina wanasema kuwa, Marekani imeongeza kasi katika njama na mipango yake ya kuzuia kutambuliwa rasmi Palestina katika Umoja wa Mataifa.

 

ABNA- Viongozi wa Palestina wanasema kuwa, Marekani imeongeza kasi katika njama na mipango yake ya kuzuia kutambuliwa rasmi Palestina katika Umoja wa Mataifa. Njama hizo za Marekani zinaongezeka katika hali ambayo, Kamati ya Mpango wa Amani ya Kiarabu imekubali kuwasilisha katika Umoja wa Mataifa ombi la kutaka kutambuliwa rasmi Palestina kama nchi huru. Kwa mujibu wa viongozi wa Palestina ni kuwa, hivi sasa serikali ya Marekani inahaha huku na huko ikitafuta uungaji mkono wa kupinga mpango wa Wapalestina wa kutaka nchi yao kutambuliwa rasmi katika Umoja wa Mataifa. Siasa za kutangatanga za Marekani zimeongezeka baada ya kushuhudiwa kuongezeka himaya na uungaji mkono wa kila leo juu ya suala la kuundwa na kutambuliwa rasmi dola huru la Palestina. Hayo yanajiri katika hali ambayo, mwezi ujao Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa linatarajiwa kujadili ombi la Palestina la kutambuliwa rasmi dola huru la Palestina.

maoni

Acha Maoni

*Mashamba alama ya asteriski ni hakika kuwa thamani.